June 10, 2022

Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe laagwa rasmi Dar

 Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, leo limefanya kikao chake cha 123 kilochofanyika Jijini Dar es Salaam, kikiwa ni kikao cha mwicho cha Baraza la sasa ambalo limemaliza muda wake rasmi (10 June 2019-09 Juni 2022). Kikao hicho kimehudhuriwa na Mwenyekiti mpya wa Baraza, Prof. Saida Yahya Othman aliyeteuliwa hivi karibuni na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baraza hilo limeagwa rasmi kwa hafla fupi iliyohudhuriwa na Menejimenti ya Chuo, na baadhi ya viongozi wastaafu katika nyadhifa mbalimbali waliotumikia Baraza hilo.
 
Mwenyekiti mpya wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Saida Yahya Othman, akimkabidhi zawadi mtoto wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, marehemu Prof. Mathew Luhanga. 

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akizungumza wakati wa hafla ya kuliaga rasmi Baraza la chuo hicho lililomaliza muda wake. 

No comments:

Post a Comment

Pages