June 10, 2022

T-PESA, NGASMAKE Wazindua Huduma ya Lipa Kwa Uhakika kumlinda Muuzaji na Mnunuzi

Kushoto, Mkurugenzi wa Kampuni ya T-PESA, Lulu Mkudde na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya NGASMAKE, Emmanuael Ngalya, wakikata utepe kuzindua Huduma ya Lipa kwa Uhakika jijini Dar es Salaam.


Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kupitia Kampuni ya T-PESA kwa kushiirikiana na Kampuni ya NGASMAKE wamezindua HUDUMA YA LIPA KWA UHAKIKA  yenye lengo la kumlinda muuzaji na mnunuzi kwa pamoja kwa wateja kwa njia ya simu.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa T-PESA, Lulu Mkudde amesema huduma hiyo itaenda kuwa suluhisho la wanunuzi na wauzaji wa bidhaa kwa njia ya mtandao kwani itasaidia kuondoa utapeli na udaganyifu kwa watumiaji.

" T-PESA kwa kushirikiana na NGASMAKE kwa pamoja tumefanikisha kuwezesha huduma hii ya LIPA KWA UHAKIKA ambayo ni pekee kabisa inayowahakikishia usalama wa bidhaa zao," amesema Lulu.

Amebainisha kuwa huduma hiyo iataondoa kilio cha muda mrefu cha wanunuzi wa bidhaa kutopata bidhaa zao ingawa wamefanya malipo, kwani muuzaji atatsubiri mapka mnunuzi apate bidhaa yake ndio fedha itaingia kwenye akaunti yake.

Amesisitiza kuwa mfumo utamsiadia mnunuzi fedha zake kuwa salama  hadi atatakopata bidhaa au huduma na kwamba anaweza kurudisha malipo yake ikiwa bidhaa haijawasilishwa.

Ameongeza kuwa Muuzaji tafaidika kwa uwepo wa mfumo huo kwani atakuwa na uwezo wa kiuhakika wa malipo mara tu wanapowasilisha bidhaa au huduma hivyo anauwezo wa kupokea taarifa ya malipo kabla hajatoa huduma. 

Ametoa rai kwa wanunuzi wa huduam au bidhaa kupitia mitandao ya kibiashara inayopatikana nchini kutumia mfumo huo sababu unatoa usala wa fedha za wateja huku akiwakumbusha huduma hiyo inapatikana kwa kupiga menyu *150*71# kisha kuchagua namba 4 yenye Huduma ya Lipa Kwa Uhakika.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya NGASMAKE, Emmanuel Ngalya amesema kampuni hiyo inatoa huduma ya mfumo wa kifedha unaomlinda  muuzaji na mnuunuzi kwa pamoja na kwamba kutokana na changamoto nyingi za kiusalama katika biashara ya kimtandao ikiwemo utapeli na udanganyifu wamekuja na mfumo rafiki na salama wa LIPA KWA UHAKIKA utakaosaidia kuondoa changamoto hizo na kupata bidhaa zisizo na kiwango.

Amefafanua kuwa mfumo huo unafanya kazi, mnunuzi baada ya kununua  bidhaa na kulipia T-PESA  fedha hazitaenda moja kwa moja muuzaji zitahifadhiwa  kwenye mfumo mpka pale mnunuzi atakapopata bidhaa yake na kuthibitisha bidhaa aliyoagiza ndio mfumo utaruhusu fedha hizo kwenda kwa muuzaji.

Mkurugenzi mtendaji huyo amesema mfumo huo umewekwa vizuri kwa watumiaji na endapo watapata changamoto yoyote ya aidha kukosa huduma watapiga namba maalum ya kituo cha huduma kwa wateja 0800110137 au kurasa za mitandao ya kijamii.  


No comments:

Post a Comment

Pages