HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 02, 2022

Benki ya Equity yaja na Kampeni ya Karibu Memba kuadhimisha Miaka 10 ya utoaji huduma


Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Benki wa ya Equity, Rojas Mdoe akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Karibu Memba.


Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Benki ya Equity Tanzania imezindua Kampeni ya ‘Karibu Memba’ yenye lengo la kuwashukuru wateja kwa kufanya nao huduma kwa miaka 10 toka ianze kutoa huduma hapa nchini nakusaidia pia kutengeneza ajira kwa watanzania.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Benki hiyo, Rojas Mdoe wakati wa uzinduzi huo ambapo benki hiyo imetimiza miaka 10 toka ianze kutoa huduma za kibenki kwa Watanzania.


Mkurugenzi huyo wa Uendeshaji wa Benki ya Equity amesema kuwa wateja ni sehemu ya familia yao nakwamba hali hiyo imepelekea kuwaita "memba".


“Tumewahudumia kwa muda wote na kuwa vinara katika utoaji wa huduma kidigitali kama Dunia ya sasa inavyotaka, pia benki ipo mstari wa mbele kutoa huduma mbalimbali za kifedha ikiwa ni pamoja na, utunzaji fedha, Akaunti za watoto, vikundi, mikopo mbalimbali kama ya wakulima (kilimo biashara/Agribusiness), wastaafu, wafanyabiashara kubwa na ndogo ndogo, waajiriwa, watumishi wa umma na kadhalika,” amesema Mdoe.


Nakuongeza kwamba akaunti zetu zote hazina makato ya kila mwezi na gharama za wakati wa kutoa au kutuma ni nafuu ukilinganisha na mabenki mengine,hivyo tunaendelea kuwaomba wateja wetu  waendelee kutumia kutumia huduma zetu.


Amebainisha kuwa ndani ya miaka hiyo, Benki ya Equity imeweza kutoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 430 na kubadilisha maisha ya Watanzania zaidi ya 500 kiuchumi na kijamii.


“Hivi karibuni tuliweza kuzindua mradi na taasisi mbalimbali kwa ajili ya mikopo ya wakulima tukiunga mkono Serikali katika kuhakikisha tunaipa nguvu sekta hii ya msingi katika ukuaji wa uchumi wa nchi yetu. Tuna makubaliano na taasisi mbalimbali kama Agricom na Yara ili kuhakikisha kuwa wakulima wanapata pembejeo kirahisi na kwa gharama nafuu,” ameongeza Mdoe.


Amefafanua kuwa benki hiyo imejikita katika kutatua changamoto za wananchi na itaendelea kutoa elimu na fursa mbalimbali zinazotolewa na benki kwa memba wa Tanzania na Dunia kwa ujumla.


Aidha, ametoa wito kwa wananchi wengine kujiunga na huduma za Benki hiyo ili kufurahia huduma zake mbalimbali kama za mikopo nafuu ili kuwafikia wafanyabiashara wadogo wadogo, wakulima wadogo na wakubwa, wakina mama na jamii nzima katika kuendelea kujikwamua kiuchumi.


"Benki yetu ni Benki pekee yenye huduma nafuu ambazo niza  kidigitali, hivi karibuni tumezindua kampeni yetu mpya ya Benki kidigitali inayoitwa ISHI KISASA-PESA MZIGO ikiwa na lengo la kusisitiza matumizi ya huduma za kibenki za kidigitali zinazoweza kumfanya mteja kupata huduma popote alipo bila hata kufika benki" amesisitiza Mdoe


Nakuongeza kuwa "tunatoa elimu ya uwekezaji amana, utunzaji fedha, pamoja na mikopo nafuu, hivyo hii ni fursa muhimu kwenu wananchi kwasababu mtapata uwezo wa huduma za kifedha, ushauri na elimu bora.


No comments:

Post a Comment

Pages