Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka, akitoa hotuba yake wakati akifungua rasmi warsha ya wadau wa elimu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa elimu wakiwa katika warsha hiyo.
Mbunge wa Ubungo ambaye pia ni mshauri na mtaalum wa elimu, Kitila Mkumbo, akichangia mada katika warsha hiyo..
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka (kulia), akifuatilia mada katika mkutano huo.
SERIKALI inatarajia kupata msaada wa
dola za Marekani shilingi milioni 117 sawa na shilingi bilioni 269.1 za
Tanzania kutoka Ushirika wa Kimataifa wa Kusaidia Maendeleo ya Elimu
Duniani (GPE).
Fedha hizo kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu ya Msingi na Sekondari nchini.
Akizungumza katika Warsha ya elimu iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Juni 16, 2022.
Mbunge
wa Ubungo ambaye pia ni mshauri na mtaalum wa elimu, Kitila Mkumbo
amesema Dola milioni 117 zinazotolewa na GPE zitasaidia kuboresha
mazingira ya kufundishia na kujifunza, kuwajengea uzoefu walimu, kuwapa
motisha, pia uboreshaji wa menejimenti na uongozi wa shule.
Amesema maeneo hayo yanamepewa kipaumbele kwa kuzingatia hali halisi ya mahitaji ya elimu kwa sasa.
"Serikali
imekuwa ikiwekeza fedha katika mambo mbalimbali yaliyopo katika sekta
ya elimu hivyo uchaguzi wa vipaumbele umezingatia maeneo ambayo bado
yanaonekana na mapengo ili kuongeza ufanisi katika sekta ya
elimu.”Amesema Kitila.
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Eliamani Sedoyeka
amesema GPE imekuwa msaada kwa mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania
ambayo ilijiunga rasmi 2013 na mwaka 2014 ilipata msaada wa dola milioni
94.8.
Amesema fedha hizo zilitumika katika
programu ya miaka minne iliyolenga kuongeza ujuzi kwa wanafunzi katika
stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.
Amesema
fedha zinazoombwa sasa ni awamu ya tatu zikilenga kuboresha maeneo
mbalimbali katika sekta ya elimu ikiwemo kuangalia mabadiliko ya
kimfumo pamoja na kutengeneza sera ambazo zitapelekea maboresho katika
mfumo wa elimu nchini.
Aliongeza kuwa Rais Samia
Suluhu Hassan alipoingia madarakani alisitiza juu ya kuwajengea uwezo
wahitimu katika ngazi mbalimbali kuwa na ujuzi wa uzalishajimali
utakaowawezesha kuweza kujiajiri na kuajiri wengine.
“Ili
kuyatimiza hayo serikali imejipanga katika kuhakikisha inawekeza katika
kuboresha mifumo, sera na miundombinu katika sekta ya elimu.”Amesema.
Nae, mwakilishi kutoka GPE Lusinda Ramos amesema wataendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha elimu nchini.
“Tumekuwa
tukitoa fedha kwa ajili ya kusaidia uboreshaji wa elimu tangu Tanzania
kujiunga na GPE mwaka 2014 na tutaendelea kufanya hivyo katika
uboreshaji,” – Lusinda Ramos mwakilishi GPE.
Pia ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kupiga hatua katika Sekta ya elimu ambayo matokeo yake yanaongezeka kila mwaka.
Kwa
upande wa rais wa Chama cha Wawekezaji Binafsi katika Elimu, (TAPIE),
Mahmoud Mringo, amesema jambo linalofanyika ni jema kwa kuwa serikali
inatafuta rasilimali ambazo hatuna ili tuweze kujenga uwezo sahihi wa
kuweza kuwapeleka watanzania katika elimu iliyobora zaidi na hasa elimu
ambayo itamuwezesha mwanafunzi anapohitimu shule aweze kujisimamia
mwenyewe katika maisha yake ya kila siku.
No comments:
Post a Comment