Na Mwandishi Wetu
MKUU
wa shule ya Sekondari Bunda iliyopo Wilaya ya Bunda mkoani Mara,
Charles Somba, ameitaka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kuwa
na muendelezo wa programu ya uhamasishaji kuhusu mtoto wa kike kupenda
masomo ya Sayansi.
Somba
ameyasema hayo alipokuwa anafungua programu ya kuwahamasisha mabinti
iliyoratibiwa na kuongozwa na wataalam kutoka DIT iliyofanyika shuleni
hapo ikihusisha shule nne za sekondari za Wilaya hiyo ambazo ni shule
ya Sekondari Sazila, Rubana na Nyendo Sekondari pamoja na Bunda.
"Naipongeza
Taasisi hii, hiki mnachokifanya ni kitu kizuri, maana wakati mwingine
tunafundisha hawa lakini wasipoona kwa uhalisia kama ambavyo mmekuja
hawaweki bidii ila sasa hata ninyi mabinti mmeona wamama wanasayansi
hawa hapa kazi kwenu mjitahidi," alisema.
Aidha,
Somba aliiomba DIT kupanua wigo ili kuhakikisha watoto wa kike
wanahamasika hata ikiwezekana wanapoingia kidato cha kwanza ili waweze
kuwajengea uelewa mapema na hii isiwe Bunda pekee, ikiwezekana fanyeni
kila mkoa hata nchi nzima.
Mratibu
wa program ya uhamasishaji Dk. Triphonia Ngailo alisema, kwa sasa idadi
ya watoto wa kike wanaohitimu masomo ya Sayansi bado ipo chini ambapo
takwimu zinaonesha wanawake wanasayansi ni 21% wakati wanaume ni
asilimia 79% hivyo DIT kupitia ufadhili wa Mradi wa EASTRIP wakaanzisha
programu hiyo ili wawape moyo kuwa inawezekana kwa pamoja wawatie moyo
na wapambane kuhakikisha idadi inaongezeka kwa kuwa Serikali inawajali
na imeweka mazingira wezeshi ili kuwapatieni ninyi elimu ili muweze
kunufaika na fursa zilizopo kwenye masomo ya sayansi.
Naye Mwalimu Samora Laizer wa Bunda Sekondari amefurahishwa na program hiyo kwa kuwa inaleta uhalisia wa kile kinachofundishwa.
"Hili
ni jambo jema maana wakati mwingine ukifundishwa tu bila kuona uhalisia
inapoteza nguvu ila kama walivyosikia leo itawaongezea nguvu"alisema
Laizer
Aidha, Mwalimu
Fibe Musa wa Rubana Sekondari ameishauri Taasisi kujipanga zaidi kwa
kuwa jambo hilo zuri na linawasaidia zaidi hasa wanafunzi wakishahitimu
masomo wanakuwa na mwanga wa kuchagua fani wanazozipenda.
No comments:
Post a Comment