HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 04, 2022

Tanzania inatarajia kuongeza chanjo za UVIKO-19 kupitia Mpango wa Global VAX unaoungwa mkono na Marekani


 Mkazi wa jijini Dar es Salaam akipata Chanjo ya UVIKO-19 wakati wa uzinduzi wa kitaifa wa Mpango Mkakati wa Upatikanaji wa chanjo Duniani wa dola za Marekani milioni 25. Uzinduzi huo ulifanyika katika viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam.

 

Dar es Salaam - Serikali ya Tanzania imefungua ukurasa mpya katika vita dhidi ya UVIKO-19 kwa kuzindua Mpango Mkakati wa Upatikanaji Chanjo Duniani wa dola za Marekani milioni 25, utakaowezesha upatikanaji wa chanjo.

 

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mheshimiwa Ummy Mwalimu na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright wameudhuria uzinduzi wa kitaifa wa Mpango huo katika viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam.

 

Mpango huu wa Global VAX unalenga kuongeza kasi ya upatikanaji chanjo, ukisaidia serikali ya Tanzania kufikia malengo yake ya kuwafikia asilimia sitini ya walengwa. Hasa, mpango huu utahakikisha watu ambao ni vigumu kuwafikia na waliopo vijijini wanapata chanjo; kuimairisha uwezo wa wafanyakazi wa afya’ kuunga mkono juhudi za chanjo; na kufuatilia usalama wa chanjo, takwimu na uchanganuzi.

 

Mpango huu wa Global VAX ni juhudi wa serikali ya Marekani kusaidia ufikiaji wa chanjo dhidi ya UVIKO-19 kwa asilimia sabini (70) ya watu duniani ifikapo mwaka 2022. Hii ni dhamira ya Rais Biden ya kuchangia dozi zaidi ya bilioni 1.2 za chanjo ulimwenguni kote kufikia mwisho wa mwaka 2022 na kuongeza juhudi za upatikanaji wa chanjo. Serikali ya Marekani ndiye mfadhili mkubwa kwa Tanzania na tayari imetoa karibu chanjo milioni tano hadi sasa, na zingine zikiwa njiani.

 

Kama sehemu ya juhudi hizo, mnamo March 3, 2022, wakati wa mkutano kwa njia ya mtandao kati ya Rais wa Tanzania Samia Suluhi Hassan na Msimamizi wa Shirika la USAID duniani, Samantha Power, Bi Power alitangaza mpango wa USAID kuongeza dola milioni 25 ili kusaidia Tanzania kufikia malengo yake ya chanjo ya UVIKO-19. Kiasi hiki ni pamoja na dola milioni 5.3 zilizotolewa na Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC).

 

Ufadhili huu wa jumla ya dola za Marekani milioni 42.1 ni pamoja na michango kutoka Shirika la USAID, Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), Idara ya Ulinzi ya Marekani na Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea wa Marekani kwa ajili ya Tanzania kubambana na UVIKO-19. Uwekezaji huu husaidia kuzuia, kutibu na kujifunza kuhusu ugonjwa huo.

 

Katika hotuba yake, Balozi Wright ameipongeza Tanzania kwa kuchaguliwa kuwa miongoni mwa nchi chache zilizopokea ongezeko la rasilimali hizi kupitia Mpango wa Global VAX na kusema kuwa Marekani imejitolea kuisiadia Tanzania katika mapambano yake dhidi ya UVIKO-19.

 

“Tunapokabiliana na aina tofauti za virusi vya UVIKO-19 vilivyoathiri kila nchi duniani kote, tunakumbushwa kwamba hakuna hata moja wetu aliye salama hadi tuwe salama wote. Ni jukumu letu kuhakikisha wote tunapata chanjo ya UVIKO-19,” alisema Balozi Wright.

No comments:

Post a Comment

Pages