July 15, 2022

Ujumbe wa UNDP wakutana na viongozi wa ACT Wazalendo



Na Mauwa Mohammed,  Zanzibar


Tume ya Umoja wa Kitaifa ya UNDP  imekutana na  viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo  kwa lengo la kutathmini hali ya kisisa na mwenendo wa uchaguzi nchini Tanzania.

Mwenyekiti wa Chama cha  ACT Wazalendo, Juma Duni Haji  alisema hayo mara badaa ya kikao hicho kilichofanyika katika  Ofisi Kuu ya chama Vuga Mjini Zanzibar.

Duni alisema ujumbe huo umekuja kuangalia ni maeneo gani yanaweza kusaidiwa katika chaguzi zijazo za mwaka 2025 ziwe huru na zenye kukubalika chini ya usimamizi wa Tume huru ya uchaguzi.

"Umoja wa Mataifa unaweza kutusaidi ili uchaguzi ujao uwe wa amani uwe huru na wenye kuaminika katika mwenendo wa kuendeleza siasa za kidemokrasia nchini "alisema Duni

Sambamba na hilo ujumbe wa chama cha ACT Wazalendo umeleza hali halisi ilivyo na kwamba wanahitaji kutekeleza maridhiano ya kweli yaliyokubaliwa na marehemu Seif Sharif Hamad pamoja na Rais Hussein  Mwinyi.

Nao ujumbe huo wa UNDP ukiongozwa na mwakilishi kutoka umoja wa Mataifa  bibi Akinyeni Adegbola umesema watafikisha ripoti katika ofisi yao na kueleza ni maeneo gani wataweza kusaidi ili chaguzi ziwe za amani huru na haki.


No comments:

Post a Comment

Pages