July 16, 2022

Waandishi wa habari waendelea kupigania mabadiliko ya sheria

NA MWANDISHI WETU


JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF),limeendelea na mapambano ya kudai mabadiliko ya baadhi ya vifungu katika sheria za habari kwa kuunda timu ya kusimamia mabadiliko hayo.


Timu hiyo iliyoundwa na TEF inahusisha Wahariri waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari ili kuwasimamia waandishi waandamizi watakaojikita katika mchakato huo.


Akizungumza na Wahariri walioteuliwa kuwasimamia waandishi hao jijini Dar es Salaam leo katika Ofisi za Jukwaa hilo, Mwenyekiti wa TEF Deodatus Balile amesema wanapaswa kuwa na waandishi wabobezi katika harakati hizo, hali iliyopelekea  kuundwa kwa timu ya wanataaluma ambao watawasimamia waandishi ili waweze kupita njia itakayoleta mafanikio.


Amesema timu hiyo ya wataalamu wabobezi, itasaidia kwa kiwango kikubwa kunyoosha mwelekeo na hatimaye kupata matokeo chanya ambapo uteuzi huo unalenga  kuongeza chachu ya harakati kuelekea mabadiliko ya Sheria hizo.

TEF imewataja Wahariri (mentors) hao kuwa ni Joseph Kulangwa kutoka gazeti la  Raia Mwema, Stella Aron wa Majira, Rashidi Kejo anayetokea gazeti la Mwananchi, Angela Mang’enya wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC)  pamoja na waliokuwa wahariri ambao kwa sasa ni wastaafu Joseph Nakajumo na Midladjy Maez. 


TEF imefafanuwa  kuwa Angela Mang’enya amepangwa kuwasimamia waandishi wanne Fatma Hassan Ali (Channel Ten), Kissa Daniel (East Africa TV), Faridy Mohammed (Mlimani TV), Godfrey Monyo (ITV).


Aidha Joseph Nakajumo atawasimamia Christopher James (Radio One), Salma Juma (Classic Fm), Philip Nyiti (Clouds Media) na Brumo Bomola (Radio Tumaini).


Kwa upande wa Rashid Kejo atawaongoza  waandishi Regina Mkonde (Mwanahalisi Online), Faraja Masinde (Mtanzania Digital), Brighter David (Daily News Digital) na Iddy Lugendo wa Majira.


Joseph Kulangwa amepangiwa Alex Kazenga (Jamhuri Media), Peter Elias (Mwananchi), Mery Geofrey (Nipashe) na Goodluck Hongo wa Tanzania Daima.
Waandishi wengine ni Anneth Nyoni (Tumaini TV), Humphrey Msechu (Spatklight TV), Jackline Martin (Times Majira) na Yusuph Digossi (IBN TV) watakuwa chini ya Stella Aron.

 
Kwa upande wa Maez atakuwa na kazi ya kupitia kazi na kuandika ripoti.

No comments:

Post a Comment

Pages