HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 31, 2022

WASHIRIKI 552 KUNOGESHA NANENANE KANDA YA MASHARIKI


 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge.

 

Na Julieth Mkireri

WASHIRIKI  552 wa sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi wanatarajiwa kushiriki kwenye maonyesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki yatakayofanyika Morogoro katika viwanja vya Julius Kambarage Nyerere.

Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ameainisha hayo wakati akizungumza na waandishi kuhusiana na maandalizi ambapo amesema hadi sasa washiriki 372 wamethibitisha.

Kunenge amesema maonyesho hayo yanatarajia kuzinduliwa Agost 2 na Halmashauri 34 kutoka katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Dar es Salam na Tanga zitashiriki.

"Ninawaalika wananchi wajumuike katika maonyesho haya, natarajia kutakuwa na teknolojia mbalimbali kwenye sekta hizo zitaonyeshwa njooni mjifunze kupata tija" amesema.

Amesema kauli mbiu ya maonyesho hayo kwa mwaka huu ni ajenda ya kumi ya thelathini kilimo ni biashara shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo mifugo na uvuvi.

 

No comments:

Post a Comment

Pages