Na Talib Ussi, Zanzibar
Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar Mhe. Shaibu
Hassan Kaduara ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Maji Zanzibar
(ZAWA) kutafuta mashine ya kusukumia maji.
Alisema
ni lazima mashine hiyo ipatikane haraka ili wananchi wa Kizimkazi
Mkunguni waendelee kupata huduma ya maji safi na salama.
Aliyasema
hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea kianzio cha maji katika
kijiji cha kizimkazi kifuatia wananchi wa eneo hilo kukabiliwa na
changamoto ya huduma hiyo.
Alifahamisha kwamba ametoa maelekezo hayo kwa sababu ZAWA inauwezo wa kukunua mashine na wananchi wakapata maji.
“Kama
utakumbuka kesi kama hii iliwahi kutokea Jambiani, ZAWA ni mamlaka ya
Serikali wanajua wapi watapata mashine ya maji, na Serikali ya Zanzibar
haishindi kuwaletea wananchi huduma ya maji kwasababu ya mashine moja
kuharibika"alisema.
Waziri
huyo aliyagiza ZAWA kununua mashine mbili za maji zenye uwezo wa KW 11
ili wananchi wa maeneo hayo waendelee kupata maji.
Aidha
alisema tatizo la maji litamaliza hasa baada ya kumalizika mradi
mkubwa wa maji ambao unategemewa kuwa na tangi la lita milioni tano kwa
mijibu wa watalaamu.
Alisema
mradi huo upo katika hatua ya awali na unadhamiwa na Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar lakini akitokea mfadhili Serikali itampokea lengo kuu
ni hufikisha huduma kwa wananchi wote wa Zanzibar waondokane na
usumbufu wa kutafuta maji.
Naye
Mkurugenzi rasilimali Maji kutoka ZAWA Maulidi Hassan Khamis Alisema
shinda hiyo ya ukosefu wa mji imekuja baada ya kuungua mashine moja ya
kusukumia maji.
Pia
alisema mashine iliyopo uwezo wake ni mdogo KW 9.2 ndio maanza watoa
maji kwa mgao ili kuipumzisha isijeikaungua na kupelekea wananchi kukosa
kabisa maji.
Kwa
Upande wake Farida Mohamed Khamis mkaazi wa kijiji hicho, alisema
wanapata maji kwa mgao kila baada ya siku mbili jambo ambalo halikidhi
mahitaji kutokana na umuhimu wa huduma hiyo.
No comments:
Post a Comment