Asilina Abubakar akitoa ushuhuda katika Ibada ya Sherehe ya Kumletea Chanzo Halisi Matunda ya Shamba lake, iliyofayika Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga, jijini Dar es Salaam.
Maelfu
ya Uzao wa Kanisa Halisi la Mungu Baba kutoka ndani na nje ya Tanzania
pamoja na Waalikwa wa dini na madhehebu mbalimbali, Jumapili Agosti 28,
2022 (Lango la 12 Abu,1) walihudhuria kwa kishindo Ibada ya Sherehe ya
Kumletea Chanzo Halisi Matunda ya Shamba lake, iliyofayika Makao Makuu
ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga, jijini Dar es Salaam.
Mwanzoni
mwa Ibada ya sherehe hiyo Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo, Baba Halisi,
aliwaongoza wote waliohudhuria kufanya kwanza Shukurani (Maombi) ya
kumwinua Rais Samia Suluhu Hassan ili Mungu Baba aweze kumlinda, kumpa
afya njema na kumwongezea hekima, busara na maarifa ili aendelee
kuliongoza vema Taifa.
Mbali ya kumuombea Rais Samia, pia waumini
wa Kanisa hilo wakiongowa na Baba Halisi walifanya Shukurani (maombi)
kwa ajili ya Sensa ya Watu na Makazi iliyoanza Agosti 23, mwaka huu, ili
itekelezwe kwa kiwango ambacho Serikali imekusudia hasa kwa kutambua
Sensa ni jambo muhimu kwa maendeleo ya Taifa na Wananchi wote.
Akiendelea
na Ibada hiyo, Baba Halisi kwa hekima busara na kwa mpangilio mzuri wa
maneno, alifafanua kwanza kwa kirefu sababu ya Kanisa Halisi la Mungu
Baba kuandaa Sherehe hiyo yaKumletea Chanzo Halisi Matunda na kutoa
mwaliko kwa kila mtu bila kujali dini au dhehebu.
“Hapa bila
shaka lipo swali kwamba kwa nini sote tukusanyike kumletea matunda
Chanzo Halisi bila kujali dini au dhehebu la yeyote?", Baba Halisi
akasema, kisha akalitolea ufafanuzi swali hilo akisema, huku akinukuu
maandiko;
"Sababu kubwa ni kutokuwa na tofauti ya behewa la nje
na la ndani tena (Ufunuo 11:1-3). Waliotumwa walikuwa hawaruhusiwi
kutoka nje ya kuta nne maana iliandikwa hivyo. Kwa kuwa yupo Chanzo
Halisi mwenyewe ndani ya Moyo wa kila anayetenda haki (Isaya 57:15) yeye
hazuiliwi kupima chochote. Maana katika Zekaria 14:9, yeye ni mmoja na
jina lake ni moja,”akasema Baba Halisi.
Huku baadhi ya Uzao
(Waumini) wakinukuu maneo yake kwa kuandika katika 'Note book' zao,
Baba aliendelea kutaja sababu nyingine inayosababisha Kumletea Chanzo
Halisi Matunda ya Shamba lake ifanyike bila kujali dini wala dhehebu
akasema;
"Ni kwamba ile barabara (njia) ya Mwafrika kuabudu na
Muashukuru pamoja, tayari (Isaya 19:23-25). Iliandikwa kuwa itakuwepo
barabara itokayo Afrika kwenda hadi Ashuru, yaani Uarabuni ambayo ni
lugha safi (Sefania 3:10)", akasema Baba Halisi kisha akafafanua
kwamba hiyo barabara tayari ni lugha ya Kiswahili ambacho kimeenea kila
mahali na kwamaba hiyo ni sababu ya tatu ambayo inayofanya watu wote
kumletee Chanzo Halisi matunda ya shamba lake.”
Baba Halisi
ametaja sababu nyingine ni Majira ya Simba na Ng’ombe kulisha pamoja
akinukuu (Isaya 11:7-9/Isaya 2:4), Majira ya Kitabu cha Mwanzo hadi
Ufunuo wa Yohana na kwamba aliyekuwa anamiliki kila kitu ni Ibilisi kwa
mujibu wa Luka 4:5-9.
“Sasa kila kitu kimerejea kwa Chanzo Halisi
kwa mujibu wa Rumi 11:36. Ilikuwa ni lazima tumletee Chanzo Halisi
matunda ya shamba lake maana yeye anamiliki kila kitu kwa sasa na zaidi
amewaponya mengi bila kujali dini wala dhehebu.
Sababu nyingine
ni kutokuwepo tena na njia mbaya za kupata utajiri. Wakati wa Majira
saba ulikuwa huwezi kupata kitu kizuri mpaka utoe kafara kulingana na
kitu unachokitafuta.
Sasa kwa Chanzo Halisi hata kama uliua mke
au mtoto, Chanzo Halisi amekushika mkono ili yeye ndiye aonekane kwa
kila kitu unachofanya. Usiogope tena kwa kujiuliza kuwa nitaanzaje
kunyoosha wakati nilishakukosea , unapomtolea matunda leo, njia mbaya ya
dunia ambayo ilikuwa na madai kwako haipo tena,” akasema Baba Halisi.
Kuhusu
Tanzania, Baba Halisi alisema, kuna mambo mazuri na makubwa yametokea
katika Taifa hilo, lakini bado Watanzania hawajamshukuru aliyewafanyia
hayo kama inayoelekezwa katika maandiko.
"Tumepata viongozi wema,
tuna amani, Uchumi umeimarika, tumepona janga la kimbunga job, tumepona
milipuko ya magonjwa kama corona, tumepona njaa, tumepona mgao wa
umeme, tumepona ukame, tumepona jangwa, tumepona maandamano ya vurugu
mitaani, tumepona volcano, Taifa tumevuka, na kadhalika.
Kwa
haya machache na mengine mengi ni vema wote bila kujali kusanyiko la
dini au dhehebu la yeyote, kukutana kama hivi kushukuru aliyetuponya kwa
mujibu wa Efeso 4:6, ‘‘kuna Mungu mmoja na Baba wa wote, ambaye yuko
juu ya wote, anafanya kazi katika yote na yuko katika yote’’.
Mwishoni
mwa Ibada hiyo Baba Halisi aliwashukuru (Uzao) na Makuhani wa Kanisa
Halisi la Mungu Baba pamoja na waalikwa wa madhehebu na dini zote, kwa
kujumuika kwenye sherehe hiyo ambayo alisema yeye binafsi imemfanya awe
mwenye furaha kubwa na anaamini hata wengine nao wamefurahi.
Baba
Halisi alieleza kufurahishwa kwake na wote waliohudhuria sherehe hiyo
ambapo katika kudhihirisha furaha yake hiyo alitoa zawadi kwa
wahudhuraji mbalimbali akiwemo Kuhani wa Kanisa Halisi Kituo cha Kenya
ambaye alimpatia zawadi ya 'CD' ya Ibada ya Jumapili iliyotangulia
akisema anampatia zawadi hiyo kwa Kenye kufanya Uchaguzi wake Mkuu kwa
Amani na Utulivu.
“Leo nimefurahi sana kwa wote mliohudhuria
sherehe hii ya Kumeleta Chanzo Halisi Matunda ya Shamba lake bila kujali
dini au dhehebu.”
Matunda aliyopelekewa Cahanzo Halisi kaatika
Sherehe hiyo yalikuwa katika mafungu 6, yakiwa ni; Matunda ya Chanzo
Halisi, Matunda ya kujenga Moyo, Matunda ya Chanzo cha Sauti, Matunda ya
Limbuko, Matunda ya jamii na Matunda ya Shukurani.
Baadhi ya
waliohudhuria Sherehe hiyo ni Wakuu wa vyombo vya huduma Mkuu wa Kituo
cha Polisi cha Mbweni, Kamishna Msaidizi wa Polisi Ndugu Buchuma ambaye
alipokaribisha kuzungumza alisema, amependa yanayofanywa na Kanisa
Halisi la Mungu Baba kwa sababu nyingi ikiwemo kuiweka jamii pamoja hasa
Vijana.
Alisema, pia analipongeza Kanisa hilo kwa kaulimbiu yake
ya 'Ibada ni Uzalishaji' inayohiliza kila mtu kufanyakazi na kaulimbiu
ya 'Upendo usiobagua', inayohimiza watu wote kupendana bila kujajali
dini au madhehebu yao.
No comments:
Post a Comment