Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Dk. Selemani Jafo, akizungumza na wananchi wilayani Kisarawe wakati wa zoezi
maalumu kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kushiriki katika Sensa ya Watu
na Makazi.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge, akizungumza na wananchi juu ya umuhimu wa kuhesabiwa katika Sensa.
Na Victor Masangu, Pwani
MJUMBE
wa Kamati ya Sensa kitaifa na Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Dk. Selemani Jafo amewataka wananchi kutowabughudhi
makarani wa sensa na badala yake kuwapa ushirikiano wafanikishe shughuli
hiyo
Aidha Dk Jafo amesema kamati imeridhika na maandalizi ambayo yamefanyika kwa makarani na vifaa vinavyohitaji.
Dk
Jafo aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza kwenye Tamasha la sensa
lililoandaliwa na mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuhamasisha wananchi
kujitokeza kuhesabiwa ambalo limefanyika Kisarawe.
Waziri
huyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kisarawe alisema makarani wa
sensa wananchi wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa kuwapa taarifa
zinazotakiwa makarani wa sensa badala ya kuwabughughi.
"
Tuwape ushirikiano kwa kila wanachohitaji tusipowqpa ushirikiano
itakuwa haina maana kutokana na maandalizi yaliyofanyika katika shughuli
hii ya sensa, na tutambue kujua idadi itarahisisha serikali katika
kwenye utekelezaji wa miradi" alisema
Kwa
upande wake Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge ametoa onyo kwa
wanaotaka kutumia sensa kuhalifu kwamba watashughulikiwa kwa mujibu wa
sheria.
Kunenge
alisema hali ya usalama imeimarishwa hivyo wananchi waondoe hofu kwani
yeyote atakayejaribu kuharibu shughuli ya sensa hatua zitachukuliwa.
Kwa
mujibu wa Kunenge maandalizi ya mkoa huo yamefikia asilimia 96, na
uhamasishaji umefanyika kwa njia tofauti ikiwemo ya michezo na matamasha
mbalimbali kwenye wilaya za mkoa huo.
No comments:
Post a Comment