Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam kuhusu taarifa ya utendaji na vipaumbele vya mfuko huo kwa mwaka wa fedha wa 2022-23.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Mfuko
wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umesema kuwa katika mwaka wa fedha
ulioishia Juni 30, 2022 umekusanya Sh trilioni 1.42 ukilinganisha na Sh
trilioni 1.38 waliyopanga kukusanya.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha
Mshomba wakati akitoa taarifa ya utendaji na vipaumbele vya mfuko huo
kwa mwaka wa fedha wa 2022/23.
Amebainisha kuwa
wamekusanya kiasi hicho cha fedha kutokana na uboreshaji wa huduma zao
ikiwemo matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na
kwamba mwanachama anaweza kupata huduma bila kufika ofisi za NSSF kwa
kutumia mifumo ya waajiri na wanachama.
" Ili
tuweze kulipa mafao ya wanachama lazima tuwekeze michango yao kwenye
miradi salama tukifanikiwa kwenye hilo mfuko utaendelea mafao ya wateja
bila kupokea malalamiko," amesema Mshomba.
Amesisitiza
kuwa katika mwaka wa fedha 2022/23 mfuko huo umepanga kutekeleza
vipaumbele mbalimbali ikiwemo kuongeza idadi ya wanachama kuifanya NSSF
iendelee kukua na kua endelevu, kuimarisha mifumo na udhibiti wa
ukusanyaji michango kwa kutumia TEHAMA pamoja na kutoa mafunzo kwa
wafanyakazi wao.
Ameongeza kuwa watawekeza
kwenye miradi salama ili kuepusha upotevu wa fedha za mfuko pamoja na
kukamilisha miradi iliyokwishaaza ikiwemo Mradi wa Jengo la Biashara
Mwanza, Jengo la Mzizima na Miradi ya Nyumba za Makazi zilizopo
Kigamboni na Tuangoma.
Amefafanua kuwa
vipaumbele vingine ni kutekeleza mkakati wa mpango wa uchangiaji kwa
hiari hasahasa kuongeza wanachama wasio kwenye sekta rasmi na utoaji
elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa mfuko wa jamii.
Pia
amesema watapitia mpango wa maendeleo ya muda mrefu utakaoishia mwaka
wa fedha huo na kutilia mkazo miradi ya mfuko huo iliyokwishaanza ina
thamani yake ni Sh Bilioni 691.
Katika hatua
nyingine, amesema thamani ya mfuko imekuwa kwa kasi ukilinganisha na
miwili iliyopita ilikuwa Sh Bil 4.3 ambapo hivi sasa imefikia Sh
trilioni 6.2.
Amewahamasisha Watanzania
kushiriki kwenye Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23 mwaka
huu kwa ajili mipango ya mendeleo ya nchi.
No comments:
Post a Comment