HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 07, 2022

Tigo, Boomplay zaungana kunufaisha wasanii Bongo

 Na Mwandishi Wetu

 

WASANII wa muziki nchini wamezidi kupata wigo wa kutangaza kazi zo baada ya kampuni ya huduma za simu ya Tigo a kampuni ya muziki mtandaoni Boomplay kuungana kwa ajili ya kuwapa fursa wapenzi na mashabiki wa muziki kusikiliza mtandaoni.


 

Akizungumza na waandishi wa habari, mmoja wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya Mario alisema huduma hiyo mpya ya kusikiliza muziki kupitia mtandao kwenye ‘App’ ya Boomplay itazidi kuwatangaza wasanii na kuwaingizia kipato kutokana na kazi zao kusikilizwa.

 

Alisema kupitia kampeni mpya ya tigo ya ‘Wakishua; mashabiki wa muziki watapata fursa kupakua na kusikiliza muziki wa wasanini mbalimbali.

 “Binafsi nawashukuru sana Tigo na Boomplay kwa kuja na huduma hii ambayo ni fursa mpya kwa wasanii kuingiza kipato na kujitangaza Duniani kote.

 

Kwa upande wake, Meneja  Mkuu wa Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli alisema  mpaka sasa kuna watu milioni 70 Duniani kote anaotumia Boomplay hivyo kuwapo kwa huduma hiyo kutatoa fursa kwa wasanii lakini pia mashabiki kusikiliza nyimbo wazitakazo mtandaoni.

 

“Muungano huu na Tigo utatoa fursa kwa watumiaji wa huduma za kampuni hii ya simu hapa Tanzania kuwasikiliza wanamuziki wao pendwa,” alisema, Natasha.

 

Aidha, kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tigo, William Mpinga, aliema mtandao wa Tigo umekuwa ukisaidia tasnia ya muziki kwa kutoa fursa kwa wasanii kuungana na mashabiki zao.

 

“Kupitia kampeni yetu ya ‘Wakishua’ mashabiki wetu watapata hii huduma kwa gharama ile ile, lengo ni kuhakikisha Tigo inawasogeza wasanii karibu na mashabiki wao,” alisema Mpinga.

 

Kampeni hiyo imezinduliwa rasmi jana jijini Dar es salaam katika hafla iliyoudhuriwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipyya.

No comments:

Post a Comment

Pages