Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Utalii Mhe. Shaban Shekilindi (kulia) akizungumza mara
baada ya mara baada ya Kamishna Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi
kuwasilisha taarifa utekelezaji wa majukumu ya TAWA kwa Wajumbe wa
Kamati hiyo ambapo ameipongeza TAWA kazi nzuriWaziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana akizungumza
leo Jijini Dodoma wakati wa kikao na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakati wa uwasilishaji wa
utekelezaji wa majukumu ya TAWA
Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Mamlaka
ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa kuuza vitalu vya
uwindaji vipatavyo 64 kwa njia ya mnada wa kielektoniki kwa ufanisi.
Uuzaji huu unaifanya TAWA ifikie asilimia 79 ya vitalu vyote vya
uwindaji vilivyouzwa.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Shaban Shekilindi (Mb) ametoa pongezi
hizo leo Oktoba 26, 2022 Jijini Dodoma mara baada ya Kamishna
Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi kuwasilisha taarifa utekelezaji wa
majukumu ya TAWA kwa Wajumbe wa Kamati hiyo
'
Mimi pamoja na Wajumbe wa kamati hii tunajisikia fahari sana kwa hatua
hii ambayo TAWA mmeifikia kwani suala hili la kuanzishwa kwa mnada wa
kielektoniki wa vitalu vya uwindaji wa kitalii lilikuwa na kelele nyingi
kutoka ndani na nje ya nchi '' amesisitiza Mwenyekiti huyo Shekilindi
Ameeleza
kuwa mchakato wa kuanzisha mnada wa kielektoniki wa vitalu hivyo
ulipigwa vita sana na baadhi ya Wafanyabiashara wakubwa waliokuwa
wametawala katika biashara hiyo hivyo hawakutaka njia hiyo kwa hofu ya
kupoteza vitalu walivyokuwa wamevimiliki kwa muda mrefu ila kutokana na
uongozi thabiti wa Wizara ya Maliasili na Utalii hawakurudi nyuma"
Kwa
upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana
amesema zoezi hilo kwa kipindi kirefu kabla ya kuanza kutumika kwa
mfumo huo lilikuwa likikikumbwa na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa
kanuni na taratibu huku akibainisha kuwa matumizi ya mfumo wa
kielektroniki yameifanya biashara hiyo itulie na sasa hakuna kashfa
yoyote katika vitalu vilivyouzwa
''Kwenye
mnada wa kiekektoniki, wafanyabishara wa vitalu vya uwindaji
wanashindana kupitia mtandao tofauti na zamani ambapo wafanyabiashara
walikuwa wanakutana ana kwa ana na Watendaji wa Wizara'' amesema Balozi
Dkt. Pindi Chana.
Ametumia
fursa hiyo kuishukuru Kamati hiyo kwa uongozi madhubuti wa kulisimamia
suala la kuanzishwa kwa mfumo huo hali iliyopelekea Serikali kuongeza
mapato.
Amefafanua kuwa
kwa sasa hakuna kelele kwani Wafanyabiashara wa vitalu vya uwindaji wa
kitalii wameanza kuelewa lengo la Serikali na kwamba hali hiyo ya mnada
imesaidia kuwaibua wafanyabishara wadogo wanaoibukia katika biashara
hiyo kwa kuwa minada hiyo imekuwa huru na inampa fursa mtu yeyote
kushiriki.
Katika hatua
nyingine Balozi Dkt. Pindi Chana amesema vitalu 24 bado havijauzwa
akieleza kuwa hivi karibuni utatangazwa mnada mwingine kwa ajili ya
vitalu vilivyobaki.






No comments:
Post a Comment