October 06, 2022

Waziri Mkuu azitaka Asasi za kiraia kufungua akaunti katika benki za nchini

 


Meneja Mwandamizi Mahusiano Benki ya NMB, Bi. Dorah Monyo (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Mhe. Kassim majaliwa (kulia) alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya Jukwaa la mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali – Dodoma. 


Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akijadiliana jambo na wafanyakazi wa Benki ya NMB alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya Jukwaa la mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali lilolofanyika Jijini Dodoma. Benki ya NMB ni mmoja wa wadau wa jukwaa hilo. 


Na Mwandishi Wetu


Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini yameagizwa kufungua akaunti zao katika benki za nchini na kitendo hicho kimetajwa kama ni sehemu ya uzalendo.


Wito huo ulitolewa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wananchi na watumishi wa Benki ya NMB alipotembelea banda la benki hiyo katika kilele cha Jukwaa la Mwaka la mashirika yasiyo ya kiserikali.


Waziri Mkuu alitembelea NMB kuanza mazungumzo na mashirika yasiyo ya kiserikali kote nchini ili kuwafungulia akaunti ndani ya benki hiyo ambayo ina matawi 228 nchi nzima na kusema mpango huo mbali na kuonyesha uzalendo, lakini itasaidia kuongeza mzunguko wa fedha ndani ya nchi, jambo litakalotafsiriwa kama kitendo cha kizalendo.


Meneja Mwandamizi wa Mahusiano wa benki ya NMB, Bi. Dorah Monyo alisema utaratibu wa kuweka fedha kwa benki za ndani utakuwa na faida kubwa kwa wananchi kwani mzunguko wa fedha unabaki ndani na kumuahidi kuwa NMB itakuwa benki ya kwanza kusaidia mashirika hayo kuwa na akaunti ndani ya benki na zenye uendeshaji wa gharama nafuu.


Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali, Dk Lilian Badi alisema ni wakati kwa taasisi binafsi kuwekeza fedha zao kwa mabenki ya nyumbani ili kuchangia ukuaji wa uchumi.Lakini pia, aliiomba Serikali kuzipa nafasi taasisi zisizo za kiserikali ikiwemo kuwapa uhuru wa kufanya majukumu yao kwan kwa sasa wamebanwa hasa kipengere cha usajili wa miaka 10 kwani kinawakosesha nafasi ya kujadiliana na wadau kuhusu miradi mikubwa.

No comments:

Post a Comment

Pages