HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

October 27, 2022

YANGA YACHOMOKA KWA KMC NA POINT TATU



Na Mwandishi Wetu

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NPL) Yanga wameibuka na point tatu muhimu dhidi ya KMC FC katika Dimba la Benjamin Mkapa.

Haikuwa mechi rahisi kwa kwa Yanga kutokana na kuzidiwa katika maeneo mengi ya mchezo kwa dakika 90.

KMC walikuwa bora sana katika kuzuia na kaunzisha mashambulizi ya kushitukiza huku wakitawala Dimba la kati chini ya Baraka Majogoro,Nzigamasabho Steve, Emmanuel Mvuyekule na Awesu Awesu.

Bao la jioni la Feisal Salum limetosha kuwapa Yanga point tatu muhimu katika mechi ngumu, mchezaji Mkubwa katika kuamua mechi ngumu akitokea benchi na kuchukua nafasi ya Tuisila Kisinda.

Mpango wa KMC kuutawala mchezo ulikwma baada ya Kocha Nabi kufanya mabadiliko na kuongeza idadi kubwa ya viungo Ili kuweza kuwa na namba sawa ya wachezaji dhidi ya KMC.

Akitoka Bakari Mwamnyeto, Dickson Ambundo, Tuisila Kisinda, Gael Bigirimana na nafasi zao kuchukuliwa na Feisa Salumu, Denis Nkane, Aboubakary Salum na Zawadi Mauya.

Kipindi cha kwanza Yanga walikosa mipango Kwa kulazimisha KUTAKA kucheza kupitia kwenye mistari ya ulinzi ya KMC.

Stephan Aziz Ki alikuwa anakosa ufanisi kwa kulazimishwa kucheza pembeni ya mstari wa mstatiri ama mbele ya viungo wa KMC jambo ambalo liliwafanya KMC kutoapata tabu kuizuia Yanga.

Kmc ilikosa ufanisi baada ya kuchukua mchezo dakika 15 za mwisho za kipindi cha kwanza.

Viungo wa ushambuliaji wa KMC walikuwa nanmikimbio mingi sahihi na kuzama kwenye mashimo yaliyokuwa yanaachwa wazi na mabeki wa Yanga.

Emmanuel Mvuyekure, Matheo Anthony, George Makang'a walizima kiungo cha Yanga chini ya Yannick Bangala na Gael Bigirimana.

Kwa matokeo hayo Yanga wanakwea kileleni mwa msimamo wa NPL Kwa kufikisha point 17 katika michezo saba walishuka Dimbani wakishinda mitano na sare mbili.

No comments:

Post a Comment

Pages