HABARI MSETO (HEADER)


November 18, 2022

  Balige asifu TRA kuboresha mazingira ya biashara


Kamishna wa Forodha wa mamlaka ya mapato (TRA)Said Athuman(kushoto)akimkabidhi cheti cha mlipa kodi bora kwa mwaka 2022 kwa wajasiliamali wa kati wa Wilaya ya Ilala Mkurugenzi wa kampuni ya Chanika Poultry Farm ,Martin Balige wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa mlipa kodi 2022 jijini Dar es Salaam jana.


Na Mwandishi Wetu

 

Mfanyabiashara na mmiliki wa Chanika Poultry Farm, Martin Balige, ambaye aliibuka mshindi wa tatu kwa ulipaji kodi wilaya ya kikodi Chanika, amesema mazingira wezeshi ya kibiashara yatachochea ukusanyaji wa kodi na kukua kwa biashara.

Bali75y9 ge ametoa kauli hiyo jana jijini Dar es kwenye hafla ya maadhimisho ya kilele cha wiki ya mlipakodi mwaka 2022 iliyoambatana na utoaji wa tuzo kwa walipakodi bora ambayo iliandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Alisema utaratibu wa kutumia kikosi kazi kukusanya kodi uliokuwa ukifanywa na TRA ulikuwa kinyume na utaratibu, jambo lililosababisha biashara nyingi kudorora.

“Sasa hivi (baada ya kufutwa kikosi kazi) mazingira ya biashara yapo vizuri kwasababu tunaenda na utaratibu ikilinganishwa na wakati wa nyuma ambapo mimi kikosi kazi kilinivamia na kuifungia akaunti yangu binafsi bila taarifa, jambo ambalo liliniwia vigumu kwenye kuendesha maisha yangu binafsi na biashara yangu,” alisema.

Akizungumzia faida ya ukusanyaji wa kitaaluma, Balige alisema mapato yatazidi kuongezeka kwa TRA kwasababu mazingira wezeshi ya kufanya biashara yapo.

Balige pia alipongeza utaratibu wa TRA wa kuwashukuru na kuwapongeza walipa kodi unawatia moyo wafanyabiashara utachochea wale wasiofuata utaratibu kurudi kwenye mstari.

Katika hafla hiyo  Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alikuwa mgeni rasmi ambapo alitaka watumishi wa TRA wanaoendeleza vitsho, ubabi na kutaka rushwa kutoka kwa wafanyabiashra wachukuliwe hatua kwakuwa wanaichafua taswira ya taasisi hiyo.

Kwenye hafla hiyo ya utoaji wa tuzo kwa wafanyabiashara, Benki ya NMB PLC iliibuka kuwa mshindi wa jumla, huku Mgodi wa North Mara, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL PLC) na NMB PLC zikiibuka kuwa washindi wa tatu bora kwenye ulipaji wa kodi.

No comments:

Post a Comment

Pages