HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

November 01, 2022

CLUB AFRICAIN WATAMBA 'SHOW SHOW'' KWA MKAPA


 

Na John Richard Marwa

WAKATI Young Africans wakitamba kuumaliza mchezo hapa nyumbani hapo kesho dhidi ya Club Africain ya Tunisia, wao wamesema wako tayari kufanya kilichowaleta.


Club Africain kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Yanga SC kuwania kutinga hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF CC, wamesema wamejiandaa vya kutosha kuwakabili Young Africans.

Akizungumza na waandishi wa Habari Kocha Mkuu wa klabu hiyo Betrand Marchan amesema licha ya ubora wa kikosi cha Yanga wako tayari kupambana.

"Itakua mechi nzuri kwa sababu tuna dakika 180 za kucheza ili kuweza kutinga hatua ya makundi, tulikuwepo hapa mwezi mmoja uliopita kule Zanzibar ila sasa ni Dar es Salaam."

Tumekuja kupambana na  mpinzani ambaye ni mzuri, Yanga, ni kubwa na ni bora hivyo tumejiandaa kukabiliana na timu nzuri hapo kesho na utakuwa mchezo mzuri, kabla ya kurejeana  nao."

Nawafahamu wachezaji wa Yanga kama Fiston Mayele ambaye nilihitaji kumsajili miaka mwili iliyopita lakini akajiunga na Yanga wakati huo nilikuwa sehemu nyingine, lakini kuna Tuisila Kisinda, Jesus Moloko na wachezaji wengine wa kimataifa wanao wazuri sana." Amesema Kocha Betrand Marchan

Nae Nahodha wa klabu hiyo Nader Chandri amesema wanatambua umuhimu wa mchezo.

"Mechi ya kesho ni mechi muhimu kwetu sisi kama wachezaji, tunafahamu ukubwa wa Yanga lakini pia wana mashabiki wengi kama sisi lakini tumepata wiki mbili za kujiandaa na huu mchezo hivyo tuko hapa kuwapa furaha mashabiki wetu pia."

"Hii ni mechi nyingine kabisa, dhidi ya Kipanga tulikuwa tunahitaji matokeo pale Zanzibar lakini haikuwa vile tulitaka kutokana na changamoto ya Uwanja kuwa wa nyasi bandia." Amesema Nahodha Nader Chandri

No comments:

Post a Comment

Pages