Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akimpongeza kijana Zaidu Mbwana kutoka Tandahimba mkoani Mtwara kwa ubunifu wake wa kutengeneza mashine ya kubangulia korosho kwenye alipokutana naye kwenye ofisi za Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) jijini Dar es salaam alikotembelea kijana huyo Jumatato Oktoba 31, 2022. Wengine ni Afisa Mtendaji Mkuu wa JMKF Vanessa Anyoti.
Na Mwandishi Wetu
Rais Mstaafu Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amempongeza kijana Zaidu Mbwana wa Tandahimba mkoani Mtwara kwa ubunifu wake wa kutengeneza mashine ya kubangulia korosho, na kumtaka auendeleze na kuukuza ubunifu wake huo ili uweze kunufaisha nchi na wananchi maradufu.
Dkt.
Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa bodi ya Jakaya Mrisho Kikwete
Foundation (JMKF) ameyasema hayo Jumatatu Oktoba 31, 2022 alipokutana
na Zaidu kwenye ofisi za taasisi hiyo jijini Dar es salaam
alikotembelea kijana huyo.
Amemshauri kijana
huyo kuongeza uzalishaji wa mashine hizo ambazo zimesaidia wakulima wa
korosho wa Tandahimba wa kuwa na uwezo wa kubangua korosho hadi magunia
mawili kwa siku – kutoka ndoo moja tu.
"Nakupongeza
sana kwa ubunifu wako ambao sio tu umesaidia kuongeza tija kwa wakulima
wa korosho wilayani Tandahimba bali pia umenufaisha vijana wenzio wengi
kwa kujiajiri huku wakiongeza tija kwenye zao la korosho", alisema Dkt.
Kikwete. "Sasa angalia namna ya kukuza uzalishaji wa mashine hizo kwa
wingi ili izwanufaishe wakulima wa korosho na nchi kwa ujumla..."
Kijana
huyo, ambae yuko jijini Dar es salaam kukusanya mali ghafi kwa ajili ya
kutengenezea mashine hizo za kubangulia korosho wilayani Tandahimba,
alikuwa nyota katika kipindi cha KIJANA LEO episode ya 6,
kinachoandaliwa na JMKF, kwa kushirikiana na AZAM TV Pamoja na Ofisi ya
Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu.
Zaidu
alifuatwa wilayani kwake Tandahimba na kurekodiwa na baadaye kuoneshwa
akionesha ubunifu wake huo kupitia chaneli ya UTV namba 108 kwenye
kisimbuzi cha AZAM TV.
Kipindi cha
KIJANA LEO ni kipindi cha kipekee kinacholenga kuonyesha jitihada za
Vijana wabunifu wanaotatua changamoto mbalimbali katika jamii
kwa kutumia rasilimali zinazopatikana katika mazingira yao na kutumia
fursa hizo kuleta matokeo chanya au manufaa katika jamii zao ikiwemo
kutoa ajira kwa Vijana , huduma muhimu na kufanya kazi kwa ufanisi .
Kijana
huyo, ambaye alifurahi na kufarijika sana kukutana ana kwa ana na Dk.
Kikwete, ameishukuru JMKF, AZAM TV Pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa
fursa ya kujitangaza aliyoipata, na kusema kwamba kipindi cha KIJANA LEO
kimemuinua kiuchumi na amekua maarufu nchi nzima kwa namna ambayo
hakuitegemea asilani.
Zaidi ya hayo , Zaidu
alifurahi kukutanishwa na wabobezi wa masuala ya biashara na sheria
ambao waliweza kumpa mawazo kiundani zaidi ya jinsi gani anaweza kukuza
biashara yake Kwenda masafa marefu katika soko la ndani na nje ya nchi
kwenye ofisi za Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) jijini Dar es
salaam alikotembelea.
No comments:
Post a Comment