HABARI MSETO (HEADER)


November 18, 2022

 MBIO UCHAGUZI MDOGO RT ZASHIKA KASI

*Kallaghe aongeza joto umakamu wa rais

William Kallaghe (kulia), akizungumza na Katibu Muhtasi wa RT, Rahel Swai, mara baada ya kurejesha fomu.

 Katibu msaidizi wa DAA, Felix Chunga, akirejesha fomu kwa Katibu Muhtasi wa RT, Rahel Swai.
 


NA TULLO CHAMBO

MBIO kuwania kuziba nafasi zilizowazi Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), zimezidi kushika kasi baada ya leo wagombea kadhaa kujitosa huku aliyewahi kuwa Makamu wa Rais, William Kallaghe, akiongeza joto la ushindani.


Kallaghe ambaye aliwahi kuongoza chini ya uongozi wa Mh. Anthony Mtaka, amerejesha fomu katika ofisi za RT jijini Dar es Salaam majira ya saa 7 mchana Novemba 18, hivyo kufanya hadi sasa idadi ya wagombea nafasi ya makamu wa rais kufikia watano na kufanya king'anyiro hicho kuwa na ushidani hasa kutokana na ushawishi mkubwa aliokuwa nao.


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa RT, Lwiza John, wagombea wengine ni Kanali mstaafu Juma Ikangaa, Suleiman Nyambui, Mohammed Kiganja, Katibu Mkuu wa Riadha Dar es Salaam (DAA), Rahim Kalyango na 
Yotham Gitige.


John, aliwataja wagombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Tendaji Kanda ya Pwani, kuwa ni Tabu John Jilala Mwandu, Ally Mussa Hoza, 
Thomas Tryphone na Katibu msaidizi Riadha Dar es Salaam, Felix Chunga.

Afisa Habari huyo, alisema zoezi la urejeshaji fomu litafikia tamati Novemba 20 na kwamba hakutakuwa na muda wa nyongeza.


"Mara baada ya urejeshaji fomu kukamilika, Novemba 23 itakuwa ni usaili jijini Dodoma na kutangaza matokeo, Novemba 24 ni kupokea mapingamizi huku Novemba 25 hadi 27 ni kampeni kwa wagombea na uchaguzi wenyewe," aliongeza.
RT inafanya uchaguzi huo, baada ya wale waliokuwa wakishikilia nafasi hizo kujiuzulu kutokana na sababu mbalimbali.



No comments:

Post a Comment

Pages