HABARI MSETO (HEADER)


November 17, 2022

SIMBA YAMTAMBULISHA KOCHA WA VIUNGO


Na Mwandishi Wetu

Klabu ya Simba SC imetambulisha rasmi Kocha wa Viungo Kelvin Mandla raia wa Afrika Kusini, ambaye anajiunga na Benchi la Ufundi linaloongozwa na Kaimu Kocha Mkuu Juma Ramadhan Mgunda.

Simba SC imekua ikipitia wakati mgumu baada ya kuondoka kwa Kocha wa Viungo Sbai Karim aliyeongozana na aliyekua Kocha wa Klabu hiyo Mserbia Zoran Maki aliyetimka kutimka mwanzoni mwa msimu huu, ikiwa ni siku chache baada ya kusaini mkataba wa kuanza kazi klabuni hapo.

Katika hatua nyingine Kurasa za Mitandao za Klabu ya Simba jana zilimtangaza Kocha wa Makipa Chlouha Zakaria,

Kutambulishwa kwa Kocha huyo kunatarajiwa mabadiliko makubwa katika utimamu wa miili ya Wachezaji wa Simba SC ambao wamekua wakilalamikiwa kukosa sifa ya kuhimili upinzani kutoka kwenye timu pinzani wanazokutana nazo katika Michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment

Pages