HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

November 08, 2022

YANGA MGUU SAWA MJINI TUNIS KUWÀA CLUB AFRICAIN


Na Mwandishi Wetu

KIKOSI cha Wananchi mchana wa jana kiliwasili kwenye Mji wa Tunis kikitokea Mjini Sousse, nchini Tunisia tayari kwa mchezo wa mkondo wa pili hatua ya mtoano kuwania kutinga hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Yanga itashuka dimbani kesho mjini Tunis, ikihitaji kufanya vizuri ili kuweza kutinga hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho CAFCC baada ya kutoka suluhu mchezo wa kwanza uliopigwa Benjamin Mkapa Novemba 2, 2022.

Katika mechi hiyo ijayo, Yanga inahitaji sare ya mabao au kushinda ili kurejea rekodi ya kutinga makundi ya Shirikisho mwaka 2016 na 2018 kupitia hatua hiyo ya mtoano.


Kwa mujibu wa Nahodha Bakari  Mwamnyeto amesema wamekaa na benchi la ufundi pamoja na viongozi kuhakikisha wanafanya kilicho bora na wao kama wachezaji wanafanya kila namna kuhakikisha wanapata matokeo.

“Tuna dakika 90 ngumu, subirini muone, kwani kama wachezaji tumejiandaa na tumejipanga kufanya kilicho bora. Ni mchezo muhimu kwa kila upande kila mmoja amejiandaa, hivyo atakayefanya vizuri ndiye atakayesonga hatua inayofuata kwa upande wa viongozi, benchi la ufundi wamemaliza mambo yote kazi imebaki kwetu,”

“Tunaomba ushirikiano kutoka kwa Watanzania wenye mapenzi na timu yetu nafasi tunayo, ni suala la muda tu kila kitu kinawezekana kama wao waliweza kutuzuia nyumbani sisi tunashindwa vipi kuwazuia kwao.” Bakari Mwamnyeto.

No comments:

Post a Comment

Pages