Tanzania
Commercial Bank (TCB) Imeendelea kushiriki zoezi endelevu la ujenzi wa kipande
cha nne cha ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Tabora hadi Isaka chenye urefu wa
kilomita 165.
TCB imeshirikia kikamilifu
katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha kutoka Tabora
hadi Isaka chenye urefu wa kilomita 165..
TCB imekuwa mdau mkubwa wa
maendeleo katika sekta mbalimbali na kuhakikisha kuwa inatoa huduma stahiki
kila kona ya Tanzania na kuhakikisha inaunga mkono kwa asilimia zote maendeleo
ya nchi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi
wa wateja wakubwa wa Tanzania Commercial
Bank Adolphina William wakati wa
uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa reli ya Kisasa (SGR) awamu ya nne leo Mkoani Shinyanga
Adolphina amesema, Tanzania
Commercial Bank ni Benki ya Wananchi na wamejitoa na wameshiriki kwa hatua kubwa
katika kuhakikisha shirika la Reli Tanzania (TRC) linafanikisha mradi wa SGR kwa mafanikio makubwa.
“Tanzania commercial Bank ni
wadau wakubwa wa maendeleo hapa nchini na kuchangia ujenzi wa Taifa, TRC
wanafanya kazi nzuri sana kuhakikisha wanaunganisha wananchi kwa njia ya
usafiri wa reli hivyo mradi huu wa SGR utaleta mafanikio makubwa hapa nchini.
Adolphina ameeleza kuwa kwa
Sasa Tanzania Commercial Bank ina matawi kila pembe ya Tanzania hivyo
imejipanga vyema kutoa huduma kwa watanzania pamoja na wageni kutoka nje hivyo
amewasihi watanzania ambao bado hawajafungua akaunti na benki ya TCB wakafungue
akaunti ili kunufaika na huduma zinazopatikana katika Benki hiyo.
No comments:
Post a Comment