Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Kadhi
Mkuu wa Dar es Salaam Sheikh Ramadhani Kitogo amewataka Waislam nchini
kutambua Majukumu ya Ofisi za Makadhi na kufuata miongozo wanayopewa
katika uendeshaji wa mashauri yao.
Ameyasema
hayo wakati akiongea na wanahabari ofisini kwake jijini Dar es Salaam
na kuwataka Waumini na Waislamu kutambua Majukumu ya ofisi hizo
yanaendeshwa kwa kufuata utaratibu.
Amebainisha
kuwa suala hilo la uendeshaji limegawanyika katika mafungu matano ya
kiuendeshaji ikiwemo Mirathi ya ndoa, Nyumba za wakfu Kutoa maelekezo ya
kisheria yahusuyo uislamu sanjari na migogoro ya misikiti.
"Waislam
wanahaja ya kubadili mitazamo ya kifikra kutambua ofisi hizi
hazishughulikii utoaji wa talaka pekee bila kufuata utaratibu na
miongozo iliyowekwa ikiwemo usuluhishi na utoaji wa maamuzi ya mashauri
yao"
Amesema kwamba hatua
hizo zikifuatwa hakutakuwa na malalamiko Wala manung'uniko Kwani kila
Moja ataona haki imetendeka Kwa kujua Baraza linania nzuri ikiwemo vikao
kuanzia ngazi ya Kata nyumbani hadi kufikia katika Ofisi hizo.
"Utakuta
watu wanashindwa kufuata utaratibu wanatoa lawama za wazi Kwa mihemuko
bila kujua Ofisi hizi zinaendeshwa Kwa mujibu wa sheria za dini tujenge
hofu ya Mungu twende na utaratibu kuanzia ngazi zilizopo Ili kuwa rahisi
Kutoa maamuzi yenye tija Kwa mashauri yao" Amesema Kadhi Kitogo.
Amesisitiza
kuwa sio kila shauri linaloletwa ofisini kwake litolewe maamuzi hapo
hapo bila kufuata utaratibu kwani huko ni kuwanyima haki stahiki ya
kuwasikiliza wengine na kufanya maamuzi ya upande mmoja.
Ameongeza
kuwa tuhumu za kwamba ofisi hiyo imekuwa haiwatendei haki wakinamama
wanaoleta mashauri sio za kweli kwa mujibu wa uislamu tumekuwa tunaanzia
ngazi ya malezi hadi makuzi na uislamu upo wazi kwa miongozo na utoaji
haki.
"Haki katika
uislamu zimebainishwa wazi katika Quran na Sunah ya Mtume Muhammad
S.W.A kwa mafundisho ya wazi katika sheria za kiislamu hivyo hakuna
jipya ila utaratibu wao wa uendeshaji mashauri ni muhimu kufuatwa na
wengi watambue utaratibu huo na kuuheshimu"
No comments:
Post a Comment