HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 14, 2023

 LIVERPOOL YANYONYOLEWA NA BRIGHTON

Na Mwandishi Wetu

Majogoo wa Jiji la Liverpool wameloveshwa lovyo na vijana wa Brighton kwa mabao (3-0) mchezo wa Ligi Kuu ya England (EPL) jioni ya leo.

Unaweza sema ulikuwa mchezo rahisi sana kwa Brighton kwa namna walikuwa wanawafungua Liverpool wanavyotaka.

Brighton kuna kitu wanafanya kinaitwa " ATTRACT TO ATTACK " yani mvute mpinzani wako aje ili umshambulie : Dunk Colwill na Sanchez nyuma ndio walivyokuwa wanafanya wanakaa na mpira na kugusa mara nyingi ili Liverpool waende kufanya shinikizo kisha wanapiga pasi nyuma yao wanatoka kirahisi kwenye shape yao ya 2-4 yani. Colwill na Dunk nyuma


Mbele yao viungo wawil ( Caicedo na McAllister ) halafu Gross na Estupian ambao ni mabeki wa pembeni wanatanua uwanja pembeni.

Kama mpira ukienda kushoto basi Gross ( beki wa kulia ) anaingia ndani karibu na viungo na kama mpira ukienda kulia , Estupinian anaingia ndani karibu na viungo maana yake?

Brighton wanakuwa na watu wengi kwenye kujenga mashambulizi huku wakitengeneza njia za pasi mbele kutoka kwa mabeki wao wa kati

Mawinga wao wawili kubaki juu zaidi ya uwanja tena pembeni ( March na Mitoma ) inasaidia nini ? Ni kuwafanya TAA na Robbo kushindwa kujumuika kwenye shinikizo nyuma ya viungo wao ( Thiago Fabinho na Hendo ) na kama wakienda basi March na Mitoma wanapata 1 Vs 1 nyingi dhidi ya Konate na Matip / Gomez.

Liverpool Walikuwa dhofu bin hali, wakiwa na mpira nyuma wanapoteza kirahisi, kwenye kiungo wanashindwa kukaa na mpira safu ya ushambuliaji hawana muunganiko mzuri.


No comments:

Post a Comment

Pages