HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 14, 2023

 MAN UNITED YAITANDIKA MAN CITY OLD TRAFFORD

Na Mwandishi Wetu

Au Basi, Manchester United weshinda mabao (2-1) dhidi ya wapinzani wao wa Jiji la Manchester mtanange uliolindima Uwanja wa Old Trafford.



Kocha wa Manchester Erick Ten Hag leo aliamua kuwaachia City mpira pembeni ( Walker na Cancelo ) huku Eriksen na Martial kazi yao kufunga njia ya pasi kwenda kwa Silva na Rodri , Fred alikuwa na kazi ya kutembea na Kelvin De Bruen, wakati Bruno na Rashford wanakaa mbele ya Akanji na Ake kuwazuia wasipige pasi za mbele bali njia pekee ni kupiga mpira mrefu au kwa mabeki wa pembeni wao na United walifanikiwa sana kuwazuia City wasicheze ndani bali wacheze pembeni ambapo Malacia na Wan Bissaka hawakuwa na shida ya kupambana dhidi ya Mahrez na Foden.

United silaha yao kubwa ilikuwa nini ? 'Counter attacks' ambapo walikuwa wanawasuburi City wapoteze mpira wakiwa katikati ya uwanja au katika eneo lao wakijua Walker na Cancelo watakuwa wameacha nafasi kubwa nyuma yao na kufanya Akanji na Ake kuzuia eneo kubwa la uwanja

Kinyume chake City wakiwa na mpira wakipoteza na ukifika himaya ya United ndio shughuli imeisha na kipindi cha kwanza United wangeweza kuwaadhibu City kwa kufanya mashambulizi ya haraka ambayo yaliwafungua City

Kipindi cha pili Pep alibadilisha muundo wake katika maeneo ya kwanza na ya pili ya uanzishaji mchezo :

Kuna nyakati nyuma wanabaki wawili na mbele yao watu watatu (Akanji na Ake) halafu Walker Rodri na Cancelo ( mabeki wa pembeni wanaingia ndani ) huku KDB na Silva wanakuwa namba 10 wawili hii ilianza kuwapa tabu viungo wa United jinsi ya kuzuia na hapo ndio KDB akaanza kupata nafasi ya kushambulia nyuma ya kiungo cha United kwasababu Fred alikuwa hajui anaanzia wapi

Licha ya Man United kufungwa na kuonesha matamanio na juhudi za kurejea mchezoni na kufanikiwa kupata ushidi wa mabao (2-1) Bruno Fernandes na Marcus Rashford huku bao la City likiwekwa kambani kupitia kwa Jack Grealish.


No comments:

Post a Comment

Pages