Na Mwandishi Wetu
MKAZI wa Kibugumo Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, amehukumiwa kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka 30 baada ya kukutwa na hatia ya kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin.
Hukumu hiyo imetolewa mwishoni mwa mwaka jana Desemba 30 na Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni, iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Janeth Mgaya.
Hakimu alimtaja mashtakiwa huyo kuwa ni Ally Issa (40) maarufu kama Mpeche.
Hakimu Mgaya alisema ametoa hukumu hiyo baada ya mshtakiwa huyo kukiri kosa la kusafirisha dawa hizo za kulevya kinyume cha sheria.
Inadaiwa kuwa Ally na wenzake wawili ambao Abdulrahman Hassan (40) pamoja na Mariam Fundi (28).
walikamatwa Disemba 9, mwaka jana katika eneo la Kibugumo kwa mbuzi wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam wakiwa na gramu 75.62 za dawa za kulevya aina ya heroin na kufunguliwa kesi ya jinai namba 89 ya mwaka 2022.
Hata hivyo, washtakiwa hao wengine wawili walikana shtaka hilo, hivyo kesi dhidi yao inatarajiwa kutajwa mahakamani hapo Januari, 4 Januari 2023.
No comments:
Post a Comment