Mashirikiano ya Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) yanatarajiwa kuibua kasi ya kiutendaji katika sekta ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu ili wananchi waweze kudhimudu.
Akizungumza Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi (SMZ) Dkt. Mngereza Mzee Miraji katika kikao cha mashirikiano ya kiutendaji kilichofanyika mwisho wa wiki iliyopita katika ukumbi wa Wizara hiyo Maisara Unguja, alisema kupitia vikao vya mashirikiano baina sekta mbili hizo vitasaidia katika kuibua kasi ya utendaji hasa katika sekta ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu zenye kukidhi mahitaji ya wananchi wenye kipato tofauti.
Alisema kwamba kunamafanikio yameanza kuonekana kupitia vikao hivyo ikwemo kukamilika rasimu mbili ya makubaliano (MOU) zimekamilika kiutendaji ambapo zitarajiwa kusainiwa katika kikao kijao cha ngazi ya mawaziri wa pande zote mbili wa wizara ya Ardhi ya SMZ na SMT.
Dkt Mngereza alifafanua kwamba ‘MOU’ zilizokamilika ikiwemo ya Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC) na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na ‘MOU’ inahusu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi (SMT) ambapo kuna mambo mengi ya ushirikiano wamekubaliana ikiwemo ngazi ya kitalaamu, kubadilishana uzoefu pamoja na mafunzo kwa watendaji wa taasisi mbili hizo.
Pia alisema wizara ya Ardhi ya SMT imepiga hatua zaidi kiutendaji ambapo wanamfumo unayojulikana kwa jina la Intergreted Land Information System unasaidia kutatua changamoto ya urasimu pamoja na kuboresha huduma hivyo wizara yake kupitia Idara ya Kamisheni ya ardhi imeanza maandalizi ya kuwa na mfumo huyo na wamefika katika hatua nzuri.
Sambamba na hayo Dkt Mngereza alisema wamekubaliana wawe na mashirikiano ya tafiti katika sekta ya ardhi na makaazi ya bei nafuu lakini katika kuanzia hilo watakuwa na kamati ya pamoja (Joint committee) ambayo imeshaingizwa katika mazungumzo ya yanayoendelea baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na taasisi ya Shelterafrique.
Alifahamisha kwamba taasisi ya Shelterafrique inautaratibu wa kutoa mikopo ya bei nafuu kwa nchi wanachama zaidi ya nchi 30 na mwaka huu wanatarajia kutakua na mkutano pamoja na maonesho ya teknolojia ya ujenzi wa maakazi ya bei nafuu.
Aidha Dkt Mngereza alisema wizara yake inakabiliwa na changamoto ya wataalamu wa upimaji ardhi ndani ya maji (Hydrographic Survey) hivyo wamekubaliana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi SMZ watakuwa na mpango mkakati wa kuwajengea uwezo watendaji wao ambapo kila wizara italazimika kuingiza katika bajeti yake.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi (SMT) Dkt. Allan H. Kijazi alisema watahakikisha wanaweka misingi imara kwa watanzania wote kumiliki nyumba za bei nafuu na kuendeleza matumizi ya ardhi bila ya kuangalia tofauti yoyote.
Alieleza kwamba matarajio ya kikao hicho ni kuwa na mifumo ya pamoja ya uboreshwaji wa utoaji huduma kwa viwango vinavyofanana baina ya Taasisi mbili hizo kwa lengo la kukidhi mahitaji ya Taifa.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu Shirika la Nyumba Zanzibar(ZHC)Mwanaisha Ali Saidi kupitia kikao hicho aliwaahidi wananchi wategemee mabadiliko katika sekta ya maakaazi nakusemba kwamba Shirika lake limejipanga kimkakati katika kuhakikisha linatoa huduma ya nyumba bora na salama kwa bei nafuu.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemiah Kyando Mchechu alisema Shirika hilo kwa sasa limejikita zaidi kwenye miradi ya ujenzi ambapo ndio kipamumbele chake kujenga nyumba katika jiji la Dar es salaam, Dodoma na maeneo ya miji na nyumba hizo ni za ghoroma na bei nafuu.
Kwa upande wa watendaji waliyoshiriki kikao hicho wamezipongeza Serikali zote mbili(SMZ na SMT) kwa kuagiza kuweko na mashirikiano ya kiutendaji katika Taasisi ambazo zinalingana kimajukumu na hazimo katika orodha ya sekta ziliyomo katika Muungano.
No comments:
Post a Comment