Katika kusherekea maadhimisho ya miaka 59
ya
Mapinduzi Zanzibar, wafanyakazi wa Benki ya NMB kutoka matawi ya
Zanzibar wameungana na Baraza la Udhibiti la Mifumo wa utoaii Leseni
(BLRC) Zanzibar kufanya usafi Kwenye viwanja vya Maisara.
Hii
ikiwa ni ushiriki wao kwenye shughuli mbalimbali za kijamii zilizopangwa
na serikali katika kuadhimisha sikukuu ya Mapinduzi Zanzibar.
Benki hiyo ni mmoja wa wadhamini wa michuano ya kombe la Mapinduzi yatakayofanyika kesho uwanja wa Amaan.
Meneja wa Biashara za Zanzibar wa Benki
ya NMB, Naima Shaame (wapili kulia) pamoja na baadhi ya watumishi wa
Benki ya NMB na Baraza la Udhibiti wa Mifumo ya utoaji Leseni (BLRC)
Zanzibar wakiwa katika shuguli za kuvisafisha viwanja vya maisaraikiwa
ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 59 ya mapinduzi matakatifu
ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment