KATIBU Mstaafu wa Kamati Maalum ya NEC, Idaraya Organaizesheni CCM
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR
KATIBU
mpya wa Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Ndg.Omar
Ibrahim
Kilupi,amesema chini ya uongozi wake hakuna Chama chochote
cha
kisiasa kitakachozuia ushindi wa CCM mwaka 2025.
Msimamo
huo ameutoa leo wakati akikabidhiwa ofisi ya idara hiyo Kisiwandui na aliyekuwa Katibu wa
Idara ya Organazesheni Ndg. Galos Cassian Nyimbo huko Kisiwandui Zanzibar.
Kilupi alisema Chama hicho kina tiketi ya kudumu ya kuongoza dola kutoka kwa wananchi wanaokiamini na kukipenda kutokana na usimamizi mzuri wa Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2022.
Alifafanua kwamba CCM ni Chama mwalimu na kiongozi wa vyama vingine vya kisiasa kwani imejiwekea mfumo imara wa kiuongozi na utendaji kuanzia ngazi ya shina hadi taifa.
Alisema
kwamba CCM kupitia ibara ya 5 ya Katiba yake imeweka wazi dhamira yake ya kushinda bila
vikwazo kwa kila uchaguzi wa dola.
Alisema
idara hiyo inahusika moja kwa moja ma masuala yote ya uchaguzi hivyo jukumu lake la
kwanza ni kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Dola wa mwaka 2025.
“
Nachukua nafasi hii kwanza kukishukru Chama Cha Mapinduzi kilichoamua kunipa dhamana hii
kubwa, naahidi kutumia uwezo wangu wote kuhakikisha kinashinda kwa asilimia kubwa
katika uchaguzi
wowote
utakaotokea kuanzia hivi sasa.
Pia ofisi
yangu ipo wazi muda wote nipo tayari kushiriana na wanachama,viongozi na watendaji
wote wa CCM na wale wenye
mawazo na
fikra za kujenga chama chetu.”, alisema Kilupi.
Aidha
Kilupi aliahidi kutekeleza majukumu yake kwa uadili,ueledi na ubunifu ili kwenda sambamba na
malengo ya Chama Cha Mapinduzi.
Katika maelezo yake Katibu huyo, amewataka maofisa wa idara hiyo kuwajibika katika majukumu yao ya kikazi.
Alisema
kama dhamira ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) kinavyotaka ni kufanya kazi kwa ushirikiano na
umoja na ndiye na yeye anavyotaka maofisa
hao wa idara kuzingatia hilo.
"Kila
mtu awajibike kwenye kwenye nafasi yake na ninachoamini ni kuwa tukifanya kazi kwa pamoja
tutafanikiwa na hatutoweza kushindwa kufikia dhamira ya CCM ya kuhakikisha
ushindi wa chama kila
uchaguzi,"alisema
"Ninashukuru
kwa mapokezi yenu pia ninampongeza Katibu aliyepita Galos kwa kazi nzuri yenye
uadilifu hivyo anastahili pongezi kubwa,"alisema
Alisema
kama ilivyokawaida na desturi ya chama ni kukabidhiana vijiti vya uongozi na kinachotakiwa ni
kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.
Kupitia
hafla hiyo ya makabidhiano Ndgu.Kilupi, aliwapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kasi yao kubwa ya
kutatua changamoto za wananchi na kuwaletea
maendeleo endelevu.
Naye
Katibu mstaafu wa Idara hiyo Ndg. Casian Galos Nyimbo, amesema idara hiyo ndio chombo
mahsusi cha kufanikisha masuala yote ya uchaguzi wa Chama hivyo ni muhimu kufanya
kazi kwa juhudi kubwa.
Pamoja na hayo aliwataka watumishi katika idara hiyo kutoa ushirikiano mkubwa kwa kiongozi mpya aliyekabidhiwa ofisi ili wafikie kwa haraka malengo endelevu ya Chama Cha Mapinduzi.
No comments:
Post a Comment