Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Katika
kukuza huduma zake na kuhakikisha zinaendana na kasi ya ukuaji wa sekta
ya usafirishaji wa anga duniani, Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)
linatarajia kupokea ndege ya kwanza ya mizigo aina ya Boeing 767-300F
yenye uwezo wa kubeba tani 54 mwezi Aprili mwaka huu ambayo itatatua
changamoto ya usafirishaji mizigo hapa nchini.
Ujio wa ndege hiyo itakayokuwa mkombozi wa sekta ya usafirishaji mizigo kwa njia ya anga hapa nchini umetangazwa mbele ya wadau mbalimbali na Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu wakati akizungumza na wadau wa Usafirishaji Mizigo, wafanyabiashara pamoja na wawakilishi kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali jamesema kuwa ndege hiyo itaweka historia Afrika Mashariki na nchi Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, (SADC).
Aidha
msajili huyo wa hazina amesema kuwa hapo awali ATCL ilikuwa ikitumia
ndege abiria kusafirisha mizigo japo zilikuwa na uwezo wa kubeba tani
chache ukilinganisha na uhitaji wa soko la mizigo,hivyo ujio wa ndege
hiyo mpya ya mizigo utamaliza tatizo hilo.
Hata
hivyo katika hatua nyingine Mchechu ametoa wito kwa ATCL kuendelea
kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali nchini wakiwemo waagizaji wa
mizigo nje ya nchi na ndani ya nchi ili kutatua changamoto
zinazokwamisha ufanisi wa biashara hii pamoja na kusimamia maslahi
mapana ya pande zote yaani wadau na Serikali.
Kuhusu
mahitaji ya soko duniani amesema kwa mujibu wa Ripoti ya Soko la
Usafirishaji wa Mizigo ya 2023, ukubwa wa soko la mizigo limekua kutoka
$191.01 bilioni mwaka 2022 kufikia $199.09 bilioni kwa mwaka 2023 kwa
kiwango cha ukuaji wa kila mwaka (CAGR) cha 4.2% na ukubwa wa soko la
usambazaji wa mizigo unatarajiwa kukua hadi $224.78 bilioni mwaka 2027
kwa kiwango cha CAGR ya 3.1%.
Ameongeza
kuwa ofisi ya msajili wa hazina itaendelea kutoa ushirikiano kwa
shirika hilo ili kuhakikisha linafikia malengo yake pamoja na taasisi na
mashirika mengine ya umma.
Kwa
Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi
amesema kuwa ATCL inajivunia kwa kutoa huduma za uhakika, salama na
endelevu za ubora wa juu duniani kote.
Amebainisha
kuwa kupitia mkutano huo watachukua maoni kutoka kwa wadau wa
usafirishaji mizigo yatakayowezesha kuondoa kero na urasimu kwenye
biashara ya Mizigo.
“Yapo
mambo yanayotakiwa kufanyiwa maboresho hasa yenye urasimu lakini yapo
ambayo ni ufuataji wa sharia za kulinda usalama wa uendeshaji wa
biashara hii. Katika kikao hiki wadau watajadili na kukubaliana masuala
ya kufanyiwa kazi na kuweka malengo. Lakini pia tutaambizana ukweli kwa
wafanyabiashara ambao hawafuati sharia ambazo kimsingi ni kwa faida ya
pande zote mbili,” alisema.Imetolewa na Kitengo cha Uhusiano kwa
UmmaShirika la Ndege Tanzania (ATCL)." Amesema Matindi
Kwa
sasa ATCL ina ndege 12 na imefanikiwa kupanua mtandao wake hadi kufikia
vituo 14 vya safari za kitaifa, 8 za kikanda na 2 za mabara.
Nae,
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni, inayosafirisha mizigo ya maua, matunda,
viungo na mbegu, Amani Temu ameishukuru serikali kwa kusikia kilio chao
na inaleta ndege ya mizigo.
“Suruhisho
la changamoto tuliyokuwa nayo ni hii ndege inayokuja, kwa sisi wadau wa
sekta ya usafirishaji tunategemea kuitumi kutokana na wingi wa mizigo
na ukuaji wa sekta, tutatumia ndege hii ya mizigo.”
Awali
amesema kuwa kulikuwa na changamoto ya ukosekanaji wa nafasi za
kusafirisha mizigo kwenye ndege hasa katika kipindi ambacho kunakuwa
hakuna abiria wengi kwa sababu tulikuwa tunategemea ndege za abiria na
upatikanaji wa nafasi ya mizigo unakuwa mdogo.
No comments:
Post a Comment