Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Taasisi
ya Hakielimu imeiomba Serikali kurejea upya mapendekezo yanayotolewa
na wadau wa elimu kuhusu matumizi ya Lugha ya kiswahili kama lugha ya
kufundishia ngazi ya sekondari.
Rai
hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Dkt. Jonh Kalage
wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam kufuatia tukio la
adhabu iliyopelekea kifo cha Mwanafunzi Gloria Faustine wa Kidato cha
kwanza katika Shule ya Sekondari Mwinuko Manispaa ya Ilemela Mkoani
Mwanza.
Amebainisha
kuwa watoto wanaotoka shule za msingi na hasa za umma kuingia kidato
cha kwanza wanakua hawajawa tayari kuweza kutumia lugha ya kiingereza
katika kuzungumza na kujifunzia hivyo kutumia kiswahili kama lugha ya
kufundishia sekondari itatoa fursa kwa watoto kujifunza kwa ufasaha na
kufundishwa vema kingereza na lugha nyingine kama lugha za kigeni.
Amesisitiza
kuwa wanapendekeza dhana ya adhabu chanya kupewa mkazo katika mafunzo
darasani na kazini kwa walimu ili kuwasaidia kuepukana na matumizi ya
adhabu za kikatili akitolea mfano wakati wa mafunzo kwa vitendo kwa
walimu utoaji wa adhabu unaweza kuwa moja ya eneo la tathmini.
"
Hakielimu hatupingi kutumia lugha ya kingereza sekondari, bali
tunapinga lugha hii ya kingereza kutumika kama lugha ya kufundishia, pia
tunaendelea kusisitiza matumizi ya adhabu chanya na vichocheo chanya
katika kuimarisha nidhamu na kujifunza,amesema Dkt Kalage.
Kwa
upande wake, Mshauri Mwelekezi wa Hakielimu Wilberforce Meena
amesema.kwamba taasisi hiyo haipingi matumizi ya lugha ya kingereza
katika shule za sekondari bali lugha hiyo iwe kama lugha ya kigeni kwa
ajili ya mawasiliano huku lugha ya kiswahili itumike kama lugha ya
kufundishia.
No comments:
Post a Comment