Na Lydia Lugakila, Kyerwa
Mpango wa kuwafikisha Mahakamani wazazi wa wanafunzi 1,000 wa Sekondari ambao bado hawajaripoti shuleni Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera wafikia hatua ya mwisho ambapo tayari Mwanasheria wa Wilaya hiyo ameisha weka utaratibu wa jambo hilo.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Wialaya ya Kyerwa Benjamin Mwakasyegye wakati akitoa maelekezo ya Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo katika kikao cha Baraza la madiwani cha Robo ya Mwaka 2022/2023.
Mwakasyegye amesema kuwa tayari Serikali ilishatoa maelekezo kwa wazazi kuhakikisha wanafunzi wote wanakwenda shuleni lakini bado kuna ukaidi na kudai njia nzuri ni wazazi hao kufikishwa katika vyombo vya sheria.
"Wanafunzi 1,000 ni wengi sana hivyo sisi kama Halmashauri tumepanga na kuamua wazazi wapelekwe Mahakani tayari Mwanasheria wetu ameisha weka utaratibu" alisema Mwakasyegye.
Aidha amewataka Maafisa tarafa Wilayani humo pamoja na madiwani kuhakikisha wanafunzi wote wanakwenda shuleni Mara moja.
Katika hatua nyingine katibu Tawala huyo amewataka wananchi Wilayani humo kutumia vyema Mvua zizonyesha kwa kupanda mazao ya muda mfupi huku akiwaomba madiwani kuwaelekeza Wananchi kutumia mbolea ili kuongeza kiasi cha mavuno.
No comments:
Post a Comment