HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 05, 2023

SASA RIADHA NA WAANDAAJI DAM DAM



NA TULLO CHAMBO, RT

BAADA ya kutokea sintofahamu ya muda mrefu kati ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), na waandaaji wa matukio mbalimbali ya mbio za barabarani (RO's), hatimaye imefikia tamati.


Tamati hiyo imefikiwa baada ya kikao cha pamoja kati ya RT, RO's na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Machi 4 mwaka huu.



Katika kikao hicho kilichokuwa chini ya Makamu wa Rais wa RT na Ofisa Michezo BMT, Rahim Maguzu, kilijadili kwa kina changamoto zinzokabili pande zote tatu.


Baada ya majadiliano ya takribani saa sitaa, pande zote zilipitia vifungu mbalimbali vya kikanuni na kuafikiana kuziheshimu ili kujenga ustawi bora wa mchezo wa riadha nchini.


Kikubwa kilichokaziwa, ni waandaaji kuheshimu mamlaka zilizopo na mamlaka kutenda haki kwa wateja wao (RO's).


Kikubwa Makamu wa Rais wa RT,Kallaghe, aliwataka waandaaji kuheshimu na kushirikiana vema na vyama vya riadha vya mikoa, kwamba kuanzia hivi sasa waandaaji wanatakiwa kupata baraka za vyama vya mikoa kabla ya kuanza kutangaza matukio yao.

No comments:

Post a Comment

Pages