Na Mwandishi Wetu
Wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL hatua ya makundi Simba SC leo wanashuka dimbani Benjamin Mkapa kumenyana na Vipers ya Uganda mtanange wa kundi C wa michuano hiyo.
Simba wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo wa kwanza msimu huu dhidi ya Raja Casablanca, katika Dimba ambalo walilifanya machinjio kwa miamba mingi ya Afrika huko nyuma.
Leo ni siku ya kufanya masahihisho? Wenyewe wanasema ndio. Kwa mujibu wa Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenda kuwapa Nguvu wachezaji wao.
“Tunawaalika Uwanja wa Mkapa kwenda kwenye jambo letu. Kesho mida kama hii unakuwa umeshamaliza mipango yako alafu tunakwenda Lupaso kummaliza Vipers.
“Mechi ya mwisho hatukufanya vizuri, mechi hii twendeni tukarekebishe makosa yaliyotokea kwenye mchezo uliopita kwenye Uwanja wa Mkapa." amesema Ahmed na kuongeza kuwa.
“Twendeni tukaitafute robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, sisi hatufurahii kucheza hatua ya makundi, sisi tunaiwaza nusu fainali.”- Ahmed Ally.
Simba wasshuka kwenye mchezo wa leo wakihitaji pointi tatu pekee Ili kuendelea kujiweka sawa katika mbio za kuisaka hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo msimu huu kama ambavyo misimu mingine huko nyuma wamekuwa wakifika hatua hiyo huku msimu huu wakihitaji kuivuka licha ya kuanza vibaya.
No comments:
Post a Comment