HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 07, 2023

WANANCHI WAIFUNGIA KAZI REAL BAMAKO

 

Na Mwandishi Wetu


Wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAFCC, hatua ya makundi Yanga SC wamepania kuvunja rekodi ya mabao waliyowafunga TP Mazembe kwenye mchezo wa kwanza kwenye Dimba la Benjamin Mkapa.


Yanga kesho itashuka uwanjani kumenyana na wageni wao Real Bamako ya Mali mchezo wa nne wa kundi D ambapo mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya bao moja kwa moja.



Wananchi chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ataiongoza Yanga kuvunja rekodi yao katika michezo ya mashindano ya CAF hasa katika hatua ya makundi ambapo mara zote walizoshiriki waliishia kuvuna alama nne tu.


Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema wana kazi kubwa ya kufanya kwenye mechi za kimataifa na kupata ushindi nyumbani kutaongeza nguvu ya kufikia malengo ya kutinga hatua ya robo fainali.


“Tulishinda mabao matatu dhidi ya TP Mazembe wakasema kwamba hatuwezi kufunga mabao mengi sasa kwenye mchezo wetu ujao dhidi ya Real Bamako tunahitaji kufunga mabao mengi zaidi.


“Uzuri tuna wachezaji wazuri ambao wanafanya kazi kubwa, tunaamini kila kitu kitakuwa sawa na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu,” .


Yanga ipo kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa imekusanya pointi 4 kibindoni imecheza mechi tatu  imeshinda mmoja, sare moja na kupoteza mchezo mmoja.


Mchezo wa kwanza Uwanja wa Mkapa Yanga waliisambaratisha TP Mazembe kwa mabao  (3-1) . Kesho watakuwa na kibarua kingine nyumbani Benjamin Mkapa kukiputa na Real Bamako.

No comments:

Post a Comment

Pages