>Serikali pia kuwafikisha mahakamani kwa deni la 2.5 bilioni
Ofisa kazi kiongozi mkoa Mwanza Betty Mtega akipeana mkono na Mwenyekiti wa JOWUTA Mussa Juma alipomtembelea ofisini kwake.
Mwandishi Wetu, Mwanza
CHAMA cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) kimetangaza
kushirikiana na Kituo Cha Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC) kuwasaidia
wafanyakazi 195 wa Kampuni ya Sahara Media kudai malimbikizo ya
mishahara yao kiasi cha sh 3.5 bilioni.
Uamuzi
huo, umetangazwa Jana na Mwenyekiti wa JOWUTA Taifa, Mussa Juma na
Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa JOWUTA, Mutta Robert katika mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika ukumbi wa Chama cha Ushirika Nyanza,
baada ya kukutana na pande zote katika mgogoro huo.
Juma
amesema baada ya majadiliano baina ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na
ofisi ya Idara ya kazi mkoa wa Mwanza na LHRC wameazimia kupeleka
mgogoro huo katika Tume ya Usuluhishi (CMA)
"Kwa
kuwa mwajiri hajakaidi kulipa deni hili na ameshindwa kulipa licha ya
kuahidi kufanya hivyo hali yake ya fedha itakapokuwa nzuri, tumeona njia
bora ni kupeleka shauri hili CMA"amesema
Amesema
JOWUTA kama chama cha wafanyakazi itashirikiana na LHRC na wanasheria
wengine ambao tayari wameonesha nia Ili kuhakikisha haki za wafanyakazi
hao zinapatikana .
Juma
amesema wamefikia uamuzi ili kulinda heshma ya Tasnia ya Habari nchini,
kwani kwa sasa ni miongoni mwa sekta ambazo zinachangamoto kubwa ya
malipo na stahiki za waandishi na watangazaji kwani wengi hawana
mikataba licha ya kufanya kazi miaka mingi.
"JOWUTA
tunaamini kesi hii ya Mwanza itakuwa ni mfano wa kesi nyingine ambazo
zitafuata katika kulinda na kutetea maslahi ya wafanyakazi katika vyombo
vya habari nchini, kwani hadi sasa kuna waandishi wanaolipwa shilingi
1000 kwa habari moja na wengi hawalipwi kabisa na kubaki kutegemea
kulipwa na wanaowapa habari,"amesema
Amesema
Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari wanastahiki kupata heshma na hadhi
sawa na wafanyakazi wa sekta nyingine kwani licha ya serikali kutunga
sheria za kazi na sheria za vyombo vya habari lakini bado wanahabari
wanataabika.
"Wanahabari
licha ya kufanya kazi kubwa bado asilimia 80 hawana ajira za kudumu wala
mikataba tofauti na taaluma nyingine hali ambayo imekuwa ikiathiri
utendaji wao wa kazi"amesema
Amesema
wakati wamiliki wa vyombo vya habari wakililia uhuru wa vyombo vya
habari na kulipwa malimbikizo ya madeni ya matangazo wanapaswa kutambua
kuwa uhuru huo hautakamilika kama wanahabari wakiendelea kuwa na
maslahi duni, kufanya kazi bila mikataba na kutolipwa mishahara.
"Tunataka
katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari mwaka huu
suala la maslahi bora kwa wanahabari lipewe kipaumbele kwani uhuru wa
vyombo vya habari hauna maana kama hakuna maslahi bora kwa wanahabari,
tunaiomba serikali kuchukuwa hatua kwa wamiliki ambao hawazingatii
sheria licha ya kupata mapato katika vyombo vyao,"amesema.
Mjumbe
wa Bodi ya Wadhamini JOWUTA, Mutta Robert alisema watatumia sheria za
kazi kufungua mashauri katika vyombo vyote vya habari ambavyo havilipi
wanahabari.
"Sheria za
kazi zipo tutahakikisha tunazitumia kulinda heshma ya taaluma hii kwani
kuna wamiliki wa vyombo vya habari wanawatumia wanahabari kama vitega
uchumi vyao,"amesema
Robert
ambaye pia ni Mwanasheria amesema sheria zipo wazi na lazima zifuatwe
na wamiliki wa Vyombo vya Habari na kesi ya Mwanza itakuwa mfano kwa
wamiliki wengine ambao hawazingatii sheria za kazi.
Wakili
Hamisi Mayomba wa LHRC amesema tayari taratibu za kufungua shauri hilo
zimeanza na ambacho kinasubiriwa kukamilishwa kwa nyaraka mbalimbali
ambazo zitasaidia katika shauri hilo.
Awali
Ofisa Kazi Kiongozi mkoa wa Mwanza, Betty Mtega alisema ofisi yake
imechoshwa na mashauri ya wanahabari kushindwa kulipwa stahiki zao.
"Tumekuwa
na kesi ya Sahara Media na vituo vingine vya radio hawataki kufuata
sheria kuwalipa wafanyakazi wao licha ya kukiri kudaiwa,"amesema
Hata
hivyo amesema serikali haijakaa kimya na shauri la Sahara Media kwani
hivi karibuni litafikishwa mahakamani na ofisi ya Mwanasheria Mkuu Kanda
ya Ziwa.
"Kamishna wa
kazi nchini tayari amekamilisha taratibu zote za shauri hili kufikishwa
vyombo vya sheria na kumbukumbu zetu hadi kufikia mwezi Mei mwaka 2021
wafanyakazi 152 walikuwa wanadai zaidi ya sh 2.5 bilioni na mwajiri
amekiri kudaiwa,"amesema.
Hata
hivyo amesema deni hilo limekuwa kubwa kutokana na wanahabari kutojua
sheria za kazi kwani walipaswa kufungua mashauri mara tu wanaposhindwa
kulipwa kwa miezi miwili.
Mwenyekiti
wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Mwanza (MPC), Edwin Soko
amewataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwaamini wafanyakazi wao
kuhakikisha wanawaajiri na kuwapa mikataba bora.
"Mwanahabari
bora ni yule ambaye pia uchumi wake upo vizuri hivyo wamiliki
wakiwalipa vizuri wafanyakazi wao wataweza kufanya kazi kwa weledi
mkubwa,"amesema
Hata
hivyo Soko amewataka wanahabari nchini kujiunga na JOWUTA kwani kisheria
ndio chama pekee cha wafanyakazi ambacho kinadhamana ya kutetea maslahi
yao.
No comments:
Post a Comment