Mtunza Fedha wa Umoja wa Mitume na Manabii Tanzania, Nabii Dkt Oliva Elisha (pichani) amesema Kanisa la Mungu linahitaji matengenezo makubwa hivyo watumishi wote ambao wameitwa na Mungu wanapaswa kusoma na kusikiliza maelezo ya watumishi wengine waliowatangulia kama Mahaba wa Kiroho.
Nabii
Dkt Olivia ameyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita kando ya
kongamano la umoja wa mitume na manabii lililolenga kumshukuru Mungu kwa
mambo mbalimbali sambamba na kuangazia mafanikio ya miaka miwili ya
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan tangu
aingie madarakani ambalo limepewa jina la “Kongamano la Mshangilio”.
Amesema
kuwa watumishi wa Mungu endapo watasikilizana na kuwa na umoja thabiti
hatua hiyo itapelekea pia kuwa na mashirikiano mema na serikali katika
kutatua changamoto mbalimbali katika jamii nchini.
Ameongeza
kuwa wao kama mitume na manabii watasimama kwa imani na kwa pamoja
kumdai Mungu watanzania wote wawe salama na kuliepusha Taifa na
mmomonyoko mkubwa wa maadili uliopo kwa sasa ambao umechangia kuwepo kwa
vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto sambamba na
vitendo vya ulawiti na ushoga hivyo watashirikiana vyema na serikali
kutokomeza vitendo hivyo.
Aidha
Nabii Dkt Olivia pia amewataka watanzania kuungana kwa pamoja na Rais
Dkt Samia katika kupiga vita rushwa,ufisadi na vitendo vya ukatili wa
kijinsia katika jamii ili kuendelea kuitunza amani ya nchi ambayo
inaanzia katika ngazi ya familia.
“mimi
kama mtumishi wa Mungu kijana,nawaasa vijana kuwa Mungu anaweza
kumtumia kijana kwani kijana anaweza kufanya kazi akatengeneza
uchumi,akatoka kwenye mambo ya tamaa za kimwili hivyo vijana tufanye
kazi kwa bidii”alisisitiza nabii Dkt. Oliva Elisha
No comments:
Post a Comment