CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Ndaki ya Sayansi za Jamii waadhimisha wiki ya tafiti kwa kuandaa mdahalo pamoja na kuonesha kazi zilizofanywa na wanatasinia mbalimbali wa Sayansi za Jamii.
Akizungumza wakati wa Mdahalo jana, Mwanazuoni, Profesa Issa Shivji amesema kuwa Chuo Kikuu kilikuwa na nafasi ya kipekee katika nchi kwa kuwa Kitivo cha fikra kwa kufikiri na kusambaza Fikra hizo.
Amesema usambazaji wake ni kwa kuandika fikra bila wasiwasi, bila kudhibitiwa, uhuru wa fikra ndio ulikuwa mhimu na uhuru huo ulikuja kwa mapambano ya chuo na nchi.
"Mapambano hayo yalikuwa yanajulikana nchi nzima kutokana na mijadala yake, maandishi yaliyokuwa yanazalishwa hapa na kutokana na dhamira ya chuo kwa wananchi." Ameeleza Prof. Shivji
Amesema kuw awajibu wa wanazuoni ni sio kwa serikali wala Utawala ni kwa wanajamii, hivyo wanazuoni wanatakiwa kufanya tafiti inayohusiana moja kwa moja na hali ya wananchi.
"Kwa kuangalia hali ikoje vijijini, hali ikoje mijini, kwa kuangalia matatizo yao ni nini, madukuduku yao ni nini? na hayo yanatokana na nini? Hayo ndio maswali ya utafiti." amesema
Prof. Shivji amesema kuwa na maana si kuandika taarifa kwa serikali au kwa wafadhiri hapana, tafiti maana yake ni kufanya tafiti katika hali halisi ya wananchi hasa hali ya chini wananchi.
Ameeleza kuwa utafiti kama huo unaonyesha tumetoka wapi na tunaelekea wapi? Je, tunakoelekea ni sahihi, je utakuwa na manufaa kwa wananchi au manufaa mengine.
"Hakikisha utafiti wako yale uliyoyagundua yanawafikia wananchi wa kawaida.
Chuo ni kama kioo cha wananchi utafiti ukiwafikia wananchi, nao watajiona sura zao katika tafiti hizo." Amefafanua
Prof. Shivji amesema kuwa zikifanywa tafiti unaowashawishi wananchi, wananchi watawashinikiza serikali kutatua changamoto zao kuliko mtafiti kufanya kazi ya kuwashauri watunga sera.
Kwa Upande wa Mwenyekiti wa Mdahalo huo, Mhadhiri Mwandamizi Ndaki ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Ng'wanza Kamata amesema kuwa ya Utafiti na Ubunifu inaadhimishwa kwa sababu inahitaji uhuru na mazingira uhuru yanayoruhusu watu kufikiri bila hofu na kutafakari kwa mambo bila wasiwasi.
Amesema kuwa uhuru huo uwape wanataaluma nafasi ya kutumia akili zao kufanya tafiti zitakazoongoza mahitimisho kulingana na vitu walivyokutana navyo wakati wa kufanya utafiti bila kujali kwamba hitimisho la utafiti wao utakuwa unapendeza au haupendezi watu wengine.
"Tumeangalia uhuru wa kitaaluma na uhuru wa wanataaluma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambacho ni chuo cha kwanza katika historia ya nchi yetu, tumeweza kuona kwa nyakati mbalimbali tumekuwa na mapambano baina ya wanataaaluma ndani ya vyuo vikuu na vyuo vingine pamoja na dola.
Amesema, dola wakati mwingine inanyima uhuru wa kitaaluma na wanataaluma na hivyo wanataaluma kwa kutaka uhuru huo wamekuwa na mampambano na dola ambayo imekuwa ikiingilia uhuru huo.
Amesema nyakati zilizopita kulikuwa na mapambano hayo na kulikuwa na masuala yaliyohusu nyakati hizo lakini nayakati za sasa pia kunamasuala ambayo yanajitokeza na yanabana uhuru wa wanataaluma na shughuli za kitaaluma.
Akizungumzia suala la wajibu kwa wanataaluma amesema kuwa wanaowajibu katika jamii licha ya kuwa na mapambano ya watu katika nyakati mbalimbali wakipambana na hali walizokuwa nazo.
Akitolea mfano amesema kuwa wafanyakazi walipambana dhidi ya mameneja wanevu dhidi ya ujira mdogo.
Pia amesema kuwa wanataaluma wamekuwa wakipambania demokrasia katika nchi kwani ni mhimu kupigania demokrasia ya wakulima na wafanyakazi, wavuvi na makundi mengine ya wavuja jasho wanayo haki ya kusikilizwa na kuelekeza sera za nchi na matokeo ya sera hizo yawe na mwelekeo gani.
Kwa upande wa Mhadhiri wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt. Richard Sambaiga ametoa wito kwa jamii kutembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili kujionea kazi za tafiti zilizofanywa wanataaluma wa ndaki ya Sayansi za Jamii.
Amesema kuwa mdahalo huo ni moja wapo ya kujitathmini wenyewe wasomi katika mambo yanayowasibu katika muktadha wa kuzalisha maarifa na kuyasambaza.
"Tunapoadhimisha siku ya utafiti, Ndaki ya Sayansi za Jamii tumeamua kujielekeza kwenye masuala mazima ya Tafiti na namna ya kuzifikia jamii kwa kutatua changamoto mbalimbali." Amesema Dkt. Sambaiga
Ameeleza jitihada za wasomi katika kuendeleza ushauri na majawabu kwenye matatizo ambayo yanazikabili jamii hayafanikiwi kwa sababu utamaduni wa wafanya maamuzi kuchukua mawazo ya wasomi umepungua.
Amesema sasa ni wakati muafaka wasomi wachukue nafasi yao ya kuwaeleza watoa maamuzi kile ambacho kinapaswa kifanyike kutokana na tafiti zilizofanywa na wasomi na pengine kubuni njia mbadala ya kufikisha mawazo ya kitaaluma.
No comments:
Post a Comment