Na Victor Masangu, Kibaha
Mbunge
wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika katika kuunga juhudi za
serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta ya elimu amechangia
mifuko 100 ya sarufi kwa lengo la kukarabati miundombinu chakavu ya
madarasa Saba katika Shule ya Sekondari Visiga.
Koka ametoa ahadi ya kuchangia mifuko hiyo wakati wa halfa inayojulikana Kama Visiga day ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kuweka mikakati ya kujadili namna ya kuongeza kiwango cha ufaulu pamoja na kukutana na wazazi ili kujadili changamoto zilizopo ili zitafutiwe ufumbuzi.
Aidha
Mbunge huyo pamoja na kuchangia mifuko hiyo ya saruji ameahidi
kuchangia madawati 50 kwa lengo la kuweza kusaidia Wanafunzi kuondokana
na changamoto ya kusoma kwa mlundikano.
"Kikubwa
natambua elimu ndio kila kitu kwa hivyo nimesikiliza risala ya mwalimu
mkuu na nimegundua kuna mahitaji ambayo yanatakiwa katika kukuza kiwango
cha ufaulu kwa Wanafunzi na kuondokana na adha ya kusoma katika
mazingira ambayo sio rafiki,"alisema Koka.
Kadhalika
Mbunge huyo aliongeza lengo lake kubwa ni Kuhakikisha anashirikiana
bega kwa bega na wazazi,walezi pamoja na walimu katika kuwalinda
Wanafunzi katika kuwa na nidhani ya kusoma kwa bidiii ili kuondokana
kabisa na kupata alama mbaya.
"Kunatakiwa
walimu,walezi na wazazi kwa pamoja tushirikiane katika kuwasaidia
Wanafunzi wetu ili kutokomeza zero kabisa katika shule hii ya Visiga
sekondari na kwamba anachukukizwa na shule za kata kuitwa
kayumba,"alisema Koka.
Kwa
upande wake mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Visiga Abasi Kikonyo
katika risala yake amemshukuru Mbunge kwa sapoti yake ya kuisaidia shule
hiyo pamoja na wadau wengine wa maendeleo wakiwemo wazazi sambamba na
viongozi wa chama kwa kuchangia michango na vifaa vya ukarabati wa
madarasa.
Naye
Mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwajuma
Nyamka amesema Mbunge huyo anatekeleza ilani ya chama kwa vitendo hivyo
anastahili kuungwa mkono katika kuchochea maendeleo.
Nao
baadhi ya Wanafunzi wa shule hiyo hawakusita kutoa pongezi zao za dhati
katika kuona umuhimu mkubwa wa kusaidia ukarabati wa madarasa pamoja na
kuchangia meza na viti ambavyo vitakuwa ni mkombozi mkubwa wa kusoma
kwa mlundikano.
No comments:
Post a Comment