Rais
Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na
Mheshimiwa Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mstaafu ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Ban Ki-moon jijini Seoul, Korea Kusini
leo.Mheshimiwa Dkt. Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi yaTaasisi
ya Kimataifa inayoshughulikia Masuala ya Elimu Duniani (Global
Partnership for Education) - GPE) yuko Seoul, Korea Kusini kwa ajili ya
kukutana na viongozi wa Serikali na Mashirika Mbalimbali ya Korea Kusini
kwa ajili ya kujadili mikakati ya kuendelea kuboresha elimu katika nchi
zinazoendelea. GPE ambayo ilianzishwa na nchi za G7 miaka 20 iliyopita,
imeendelea kupigania elimu kwa ajili ya mtoto wa kike na wa kiume kwa
kuomba kuungwa mkono na nchi na taasisi zinazoweza kuchangia katika
elimu duniani.
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment