HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 25, 2023

Tuzo za Harusi Awamu ya Tatu kufanyika Mei 28

 Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


TUZO za Harusi Awamu ya tatu zinatarajiwa kufanyika Mei 28, 2023 jijini Dar es Salaam.



Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Benedict Msofe kwa niaba ya muandaaji wa hafla hiyo, amesema lengo la tuzo za Harusi ni kutambua na kusherehekea jukumu muhimu linalofanywa na wachuuzi wa Harusi Tanzania,

vile vile wauzaji na watoa huduma kwa kufanya siku za Harusi kuwa Maalum, za kupendeza, na za kukumbukwa.


“Tuzo hizi zimetengenezwa kama upanuzi wa maonesho ya Biashara ya Harusi “Harusi Trade Fair” ambayo yalikuwa maonesho ya kwanza ya Harusi Tanzania mnamo 2010 na kufanikiwa kufanywa kwa miaka nane mfululizo, maonesho ya siku mbili yaliyojazwa na wauzaji bora wa Harusi kutoka sehemu mbalimbali Tanzania na wadau mbalimbali ambao walifanikiwa kutoa duka moja kubwa kwa ajili ya mabibi Harusi, Bwana Harusi, familia na marafiki,” amesema Msofe na kuongeza,


“Tuzo za Harusi zitachunguza kwa makini ili kutambua umuhimu wa huduma zotolewazo na wafanyabiashara na watoa huduma na kupelekea ukuaji katika sekta ya Harusi Tanzania,”.


Msofe amesema kwamba kwa miaka michache iliyopita, sekta ya Harusi imekuwa na imegeuka kuwa Biashara rasmi, wastani wa Sherehe za Harusi 300 husherehekewa jijini Dar es Salaam katika kipindu cha wiki moja, hivyo kutoa maelfu ya fursa za ajira kwa wanaume na wanawake kitaifa.

Amesema wanakusudia kukuza wafanyabiashara wa Harusi na watoa huduma ili kueneza biashara na kuipa ubora sekta ya Harusi nchini.


Kwamba Mwaka 2023 kuna vipengele 21 ambavyo vitawaniwa Kati ya hivyo 19 uteuzi wake ulikuwa wazi kwa umma na ulifunguliwa Januari 20 Mwaka huu na walipokea zaidi ya majina 340 kutoka kwa vikundi 19 kupitia mitandao yao ya kijamii na ujumbe wa simu, huku vipengele viwili vikiwepo kwa ajili ya tuzo za heshima.


Ameeleza kuwa kwa sasa washiriki wanapiga kura ikiwa ni hatua moja wapo ya ushindi wao ambao husimamiwa na Kampuni ya ukaguzi ijulikanayo kama Innovex Tanzania baada ya hatua hiyo jopo la wachambuzi wa sekta ya Harusi watapitia kazi za washiriki wote ikiwa ni namna ya kuangalia ubora na ubunifu katika Kazi zao.


Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Innovex Tanzania, Bahiya Tajiri amesema kwamba kwa miaka miwili mfululizo wameshirikiana na tuzo za Harusi kuhakikisha ubora wa kura na wanaamini tuzo hizo zina tija kubwa katika jamii yetu ambayo imesababisha Mwaka huu wakubali ushirikiano huo.


Ameahidi kuwa kura hizi zitakuwa huru na za haki.

No comments:

Post a Comment

Pages