HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 24, 2023

RC Fatma Mwassa abisha hodi Kagera, aahidi kutomwangusha Rais Samia



Na Lydia Lugakila, Bukoba

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatma Mwassa, amewasili mkoani Kagera kuanza rasmi majukumu yake ya kazi, huku akiahidi kutomwangusha Rais Samia, katika kusimamia vyema miradi ya Maendeleo.



Rc Fatma Mwassa, ametoa kauli hiyo, wakati Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoani Kagera, baada ya kuwasili ambapo amesema kuwa, anamshukuru Rais Samia kwa nafasi hiyo kubwa na ya heshima ya kumuhamishia, Mkoani humo na kuwa hatomwangusha, badala yake atahakikisha anaendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na uadilifu mkubwa, akizingatia misingi ya uzalendo.

"Nianze kumshukuru Mungu kwa Afya njema, nimshukuru Sana Rais Samia kwa heshima hii, hakika sitomwangusha ninachoomba kwa Wana Kagera watumishi na Wananchi ni ushirikiano,maana maisha ya uongozi kujifunza hakuna mwisho, kila unapoendelea unapoingia Mazingira mapya ya mila tofauti, desturi tofauti na mipango tofauti ni lazima ujifunze, hivyo ushirikiano ndo kitu cha msingi" alisema Rc Fatma Mwassa.

Aidha amewaahidi Wana Kagera kuwa yeye pamoja na timu yake nzima, watafanya kazi njema sana na Maendeleo ya Kagera yataonekana.

Ameongeza kuwa fedha nyingi ambazo Rais Samia amewekeza Mkoani humo, kwa ajili ya miradi ya Maendeleo, atajitahidi kuzisimamia ili miradi itoke kwa viwango vilivyo bora, huku akiahidi kukuza uchumi wa Mkoa huo.

Ikumbukwe kuwa mnamo Mei 15, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan alifanya uhamisho wa baadhi ya wakuu wa Mikoa ambapo Fatma Abubakar Mwassa alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na  kuhamishiwa Kagera huku Albert John Chalamila alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera na kuhamishiwa Mkoa wa Dar es Salaam.



No comments:

Post a Comment

Pages