HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 20, 2023

FEI TOTO APIGA HAT TRICK AZAM IKIJIBWEDEA POINT 3

Na John Marwa

Wakati wadau na wapenzi wa soka wakijiuliza nini kitaamuliwa baada ya mchezo wa kwanza wa msimu kati ya Azam FC dhidi ya Kitayose FC kumalizika katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Ofisa habari wa Bodi ya ligi, Karim Boimanda amesema Azam wamepewa point (3) na mabao (4) yanahesabiwa. Hivyo Azam wanaongoza ligi na Feisal ndiye mfungaji kinara akiwa na mabao (3) licha ya mchezo kusimamishwa dakika ya (18').

Boimanda amesema kwa mujibu wa kanuni timu ikiwa na wachezaji (7) inaruhusiwa kucheza mchezo ndio maana waliruhusu mchezo uendelee licha ya kuwa Kitayosce walikuwa na wachezaji (8).

Ameendelea kusema kuwa, wao walipokea majina ya wachezaji (8) wanaoruhusiwa kucheza kutoka kwenye mamlaka (TFF). Wachezaji wengine wa Kitayosce wakiosajiliwa wamezuiwa kucheza.


No comments:

Post a Comment

Pages