Na Mwandishi Wetu, Tanga
MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Saddy Kambona amekutana na kufanya mazungumzo na wawekezaji kutoka nchini Nigeria ambapo amewahakikishia mazingira rafiki ya uwekezaji katika sekta ya Mkonge.
Akizungumza na wawekezaji hao ofisini kwake jijini Tanga leo Ijumaa Agosti 18, Mkurugenzi Kambona amesema wameonesha nia ya kuwekeza kwenye Mkonge.
“Kimsingi mazungumzo yetu yamekuwa na mafanikio, wao wamekuja kwa lengo la kuwekeza katika Sekta ya Mkonge wanatarajia kuanzisha mashamba na eneo la kuanzisha vituo vya uchakataji Mkonge na mnyororo mzima wa thamani katika sekta ya Mkonge.
“Nigeria ni moja kati ya nchi wanunuzi wakubwa wa singa za Mkonge (fiber) kutoka Tanzania ambapo kwa kipindi cha Januari -Machi mwaka huu iliongoza kwa kunua tani 2,071.00 sawa na asilimia 24.04,” amesema Mkurugenzi Kambona.
Pamoja na mambo mengine, Mkurugenzi Kambona amesema Bodi kama wasimamizi wakuu wa sekta ya Mkonge, iko tayari kushirikiana na wawekezaji hao kuhakikisha malengo yao yanafanikiwa.



No comments:
Post a Comment