HABARI MSETO (HEADER)


August 20, 2023

TFF, TAKUKURU ZAUNGANA RUSHWA MICHEZONI

Na John Marwa

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  (TAKUKURU) wameungana kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanamichezo kuwa na utaratibu wa kutoa taarifa kwa vitendo vinavyoashirikia Rusha michezoni.


Akizungumza na waandishi wa habari leo makao makuu ya TFF, Mkurugenzi wa Sheria, habari na masoko ya Shirikisho hilo, Boniface Wambura amesema wamekaa na Taasisi hiyo baada ya kuona changamoto kubwa katika masuala la Rushwa


Amesema wameamua kuungana na kutoa elimu kwa wanamichezo kwa ajili ya kuwaeleza juu ya athari za kutoa au kupokea rushwa na jinsi ya kuweza kufikisha taarifa hizo katika mamlaka husika.

“Tumeona hili na kuweza kufanya kampeni hii kwa wadau wetu wa mpira wa miguu kuwapa usajili wa kuweza kutokomeza suala la kupokea au kutoa Rushwa katika michezo iwe ya kiungwana.

"Kampeni yetu hiyo tuanaanza rasmi jumamosi hii kwa kuwa na bonanza la mechi kwa timu mbalimbali ikiwemo waandishi wa habari kutoka taasisi na makampuni mbalimbali pamoja na wadau wetu wa mpira wa miguu,” amesema Wambura.

Kwa upande wa Mkurugenzi  wa Elimu kwa Umma wa TAKUKURU, Joseph Mwaiswelo amesema,  kuungana na TFF ni kuimarisha furaha ya nchi kupitia mchezo wa mpira wa miguu kwani Rushwa ni adui mkubwa kwa Taifa la Tanzania.


Ameongeza kuwa wamepata chanagmoto nyingi kuhusu viashiria vya Rushwa kwenye michezo hali ambayo imewasukuma kutoa elimu kwa wadau wa soka kuweza kuwa na ujasili wa kutoa taarifa kwa kupokea au kutoa Rushwa.

“Katika michezo kuna tuhuma nyingi sana, tumelazimika kuingia katika soka kuelimisha jamii ili kupinga suala la Rushwa na kujenga ujasiri kwa wadau wa michezo ili kufanya mchezo huu kuwa wa kiungwana,” amesema Joseph.



No comments:

Post a Comment

Pages