HABARI MSETO (HEADER)


August 20, 2023

CHAMA AMKABIDHI MIQUISSONE JUKUMU ZITO

Na Mwandishi Wetu

KIUNGO wa Simba, Clatous Chama amempa jukumu kubwa mchezaji mwenzake Luis Miquissone kwa kumuambia anataka pasi 10 za mwisho kutoka kwake katika michezo iliyopo mbele yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara.



Hatua hiyo ni baada ya Chama kufunga bao la nne kwa pasi ya mwisho kutoka kwa Miquissone katika mchezo wa juzi dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao (2-4),  uwanja wa Manungu, Tuliani, Morogoro.

Chama amesema anaimani kubwa ya kufanya vizuri na kufunga mabao kutokana na muunganiko mzuri wa wachezaji wenzake hasa ikiwemo Miquissone ambaye amerejea ndani ya kikosi cha timu hiyo.

Amesema anafurahi kupata ushindi huo wa mabao (2-4) na moja akifunga akipokea pasi ya mwisho kutoka kwa Miquissone anaamini ataendelea kufanya vizuri zaidi na kufikia malengo ya timu hiyo.

“Nimefurahi kupata pasi ya mwisho na kufunga kutoka kwa Miquissone (Luis) ila nataka assist 10 kutoka kwa nyota huyo katika michezo iliyopo mbele yetu,” alisema kiungo huyo.

Amebainisha kuwa msimu huu watafanya vizuri zaidi ya uliopita kulingana na maboresho ya kikosi na kuongezeka kwa wachezaji wapya ambao watasaidia kufikia malengo yao ya kutwaa mataji yaliyopo mbele yao.

No comments:

Post a Comment

Pages