Na John Marwa
Wekundu wa Msimbazi Simba weibuka na ushindi wa mabao (2-0) dhidi ya Dodoma Jiji FC, mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NBC PL katika Dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam.
Ulikuwa mchezo wa pili na wa kwanza kwa Lunyasi kucheza nyumbani msimu huu ambapo mchezo wa kwanza walianzia Manungu Tuliani Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar ambako Simba walishinda kwa mabao (2-4).
Mchezo ulikuwa mgumu kipindi cha kwanza, kwa namna ambavyo Dodoma Jiji waliamua kucheza kwa idadi kubwa kwenye eneo lao na kuwafanya Simba kupata wakati mgumu kuwafungua.
Licha ya ugumu huo Simba walipata nafasi kadhaa na kushindwa kuzitumia ikiwemo ya Jean Baleke, Willy Essomba Onana na Saido Ntibanzonkiza.
Dakika ya 43 Simba wwalilisakama bao la kuongoza kupitia kwa Jean Baleke akimalizia pasi safi ya Mohammed Hussein Zimbwejr aliyefanya mikimbio nyuma ya safu ya ulinzi na Mzamiru Yassin kumuwekea kwenye njia.
Kipindi cha pili Dodoma Jiji walianza kuhanikiza mashambulizi wakisaka bao la kusawazisha njia iliyopelekea Simba kuanza kuutawala mchezo.
Moses Phiri 'General' aliweka kamba ya pili kwa Simba na ya ushindi akitokea benchi akichukua nafasi ya Jean Baleke sambamba na Luis Miquisone aliyechukua nafasi ya Willy Essomba Onana.
Kuingia kwa Phiri na Luis kuwalifanya Simba kuongeza kasi ya mashambulizi mengi na kutengeneza nafasi nyingi ambazo hawakuweza kuziumia vizuri.
Dodoma Jiji licha ya mpango wao kufanya kazi kiulinzi lakini matanio ya kusaka mabao uliwaweka matatani kwa sababu waliacha mianya mingi sana ya viungo wa ushamsainisha wa Simba huwa wanapend kuitumia.
Kwa ushindi huo Simba anaaa kileleni mwa msimamo wa Ligi wakifikisha pointi sita na mabao sita huku wakiwa wameruhusu mabao mawili.
Dodoma Jiji wao umekuwa mchezo wa kwanza kwao kuupoteza msimu huu ikiwa mchezo wa kwanza walianzia nyumbani dhidi ya Coastal Union na kushinda kwa mabao (2-1).



No comments:
Post a Comment