HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 21, 2023

YANGA YAWATWANGA WA DJIBOUTI KIBABE

Na Mwandishi Wetu

Mabingwa wa Tanzania Yanga SC wameshinda mabao 2-0 dhidi ya Asas FC ya Djibouti katika mechi ya hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) ikipigwa katika Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Mabao ya wananchi la kwanza  lilifungwa na Aziz KI dakika ya 22 na Kenedy Musonda akaja kumalizia bao la pili dakika ya 53.

Yanga itarudiana na Asas Agosti 26 ikiwa mwenyeji wa mchezo kwa ajili ya kupata mshindi atakayecheza hatua ya kwanza CAFCL.

Ulikuwa ushindi muhimu kwa Wananchi na sasa wanasubiri dakika 90 za pili kuweza kutinga hatua inayofuata.



No comments:

Post a Comment

Pages